Halima Mdee sasa aukana uchumba wake na Joshua Nassari...

Halima Mdee sasa aukana uchumba wake na Joshua Nassari...

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
mdeenew_314_290.jpg

Halima Mdee terms marriage vows a political ploy...........



hii ni mbaya sana kwa Halima Mdee.................kumbe akiwa jukwaani huropoka tu na wala hajali kuwa anapotosha wapigakura ili mradi apate mkate wake!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Kuanzia sasa mimi kumwamini itakuwa ni vigumu kwa sababu sijui lipi lina ukweli na lipi anajiongelea tu ili mradi aambulie mkate wake...........lol.
 
Hee!
Yamekua hayo tena ?
Imekua yale ya "chomoa nipumue!"
 
kuna mahali niliona kuwa ana katabia kabaya,
atakuwa ameshanogea hawezi kuolewa tena
 
Yaani wamemweka kati huyu dada?

Ujue kila mtu ukiwekwa kati watu wakuchambue utakutwa na mapungufu kibao kama binadamu, anyway its a free world.

Afu mkome kumfuatafuata mbunge wangu.
 
Nani wakumweka ndani mdee yule mmeru anataka ajikanumba tu.Kuna wanawake wa kuwaoa kwani hamuwajui jamani.Haya mi napita
 
kumbe watu mlilichukulia serious kiasi hiki loh hiv amuon kuwa atakabemenda katoto ka watu?
 
mdeenew_314_290.jpg

Halima Mdee terms marriage vows a political ploy...........



hii ni mbaya sana kwa Halima Mdee.................kumbe akiwa jukwaani huropoka tu na wala hajali kuwa anapotosha wapigakura ili mradi apate mkate wake!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Kuanzia sasa mimi kumwamini itakuwa ni vigumu kwa sababu sijui lipi lina ukweli na lipi anajiongelea tu ili mradi aambulie mkate wake...........lol.

Masikini Dogo Janja? Nilikuwa nishamuonea wivu hivoo, kweli kisicho riziki hakiliki.
 
kuna mahali niliona kuwa ana katabia kabaya,
atakuwa ameshanogea hawezi kuolewa tena




uliona akiwa anakafanya??
umethibitisha??
au umesikia watu wanasema na wewe ukaamua useme....
 
0.jpg


MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) amesema sasa yuko tayari kufunga ndoa na Mbunge mteule wa chama hicho wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.


“Nafurahi kwamba Nassari hatimaye ameshinda ubunge katika uchaguzi mdogo,” alisema Mdee wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa Arusha na Meru juzi katika viwanja vya Leganga kusherehekea ushindi wa chama chake katika uchaguzi huo.

Mdee alifafanua, kwamba yeye na chama chake walikuwa wamebanwa na kampeni za kuhakikisha Chadema inatwaa jimbo la Arumeru Mashariki na ndiyo sababu hakujibu mara moja maombi ya Nassari ya kumwoa aliyoyatoa katika moja ya mikutano yake ya kampeni.

“Naondoka kwenda Dar es Salaam kujiandaa kwa Mkutano ujao wa Bunge, kisha nitakwenda Dodoma ambako nitamsubiri Nassari na kwa pamoja tutafanya maandalizi,” alisema Mdee huku akishangiliwa na hadhira hiyo huku wakiimba na kucheza katikati ya mvua iliyokuwa ikinyesha.

Mdee alisema ndoa kati ya wabunge hao wawili wa Chadema ni wazo zuri na itatangazwa sana na kuandika historia.

Alipoona anashambuliwa sana na wapinzani wake juu ya useja wake katika kampeni hizo, Nassari hatimaye alitangaza kumwoa Mdee ambaye pia hajaolewa.

Na katika moja ya mikutano ya hadhara, alisimama naye jukwaani kukampeni.

“Kuna viongozi wengi wa kidini Dodoma, ikiwa ni pamoja na ndani ya Bunge ambao watatushauri jinsi ya kulitimiza hili,” alisema Mdee na kuongeza kwamba baba yake Joshua, Mchungaji Samuel Nassari alipata kusema, ‘mwanamke mzuri ni zawadi kutoka kwa Mungu’.

Chadema ina idadi kubwa ya wabunge vijana ambao hawajaoa, ikiwa ni pamoja na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Mr Sugu’; wa Ubungo, John Mnyika; wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na sasa Nassari.
 
Sijawahi kuona ukichangia mada yeyote ya maana humu jamvini zaidi ya kujishughurisha na umbea tu!.....hii sijui ni dalili gani kwa mtoto wa kiume!!!
 
Back
Top Bottom