JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee ameshauri Serikali kupunguza kodi katika ndege zinazotumika kwa utalii Nchini akisema inatakiwa kushuka na ikiwezekena ifike hatua kumiliki ndege binafsi liwe jambo la kawaida.
“Kamati imesema ndege za kukodi zimepungua kutoka 200 hadi 105, ifike kipindi Waziri Mwigulu (Nchemba), kumiliki ndege sio anasa, tuache kufikiria kimasikini, tushindanisha watu waruke hewani,” anasema Mdee akiwa Bungeni Jijini Dodoma, leo Juni 27, 2022.
Aidha, Mbunge mwingine Hamis Kigwangwalla aliongezea kwa kusema Tanzania inatajwa kuwa ni sehemu yenye gharama kubwa kufanya utalii, hivyo Serikali ishushe gharama za kupunguza kodi ikiwemo gharama za ndege kutua Nchini.