Salamu sana wanandugu?
JF ni Jumuiya kubwa sana! JF imekusanya watu wa nasaba mbali mbali! JF imebeba watu wa hadhi na rika mbali mbali! JF imebeba marafiki wa kweli, wa dhati, JF ina mpaka wanandoa wa kweli! JF ina watu wenye mahaba yao, achana na walioweka dhahiri shahiri kama
Demiss na Mkuu sana, mtu kweli, mtu mara mbili
Mshana Jr yote kwa yote JF ni kiwakilishi kizuri
cha Jamii halisi ya Kitanzania.
Napenda kuhoji hapa, nini kimewakuta wanajamii sisi? Kulikoni mpaka sasa hakuna mualiko siriazi wala hakuna alietoa ramani halisi ya kutukaribisha ndugu na jamaa huko kwenye madikodiko, maanjumati, mapilau pilau?
Haiwezekani kuwa eti Majiko ya Wana JF leo hayapikiki? Sio kweli! Haiwezekani wanaJF wote leo mmealikwa, kwamba eti na nyinyi hamuwezi kualika mlikoalikwa! Shabash.... huu ukimya kuna nini huko? Mnakula nini hicho kisichofaa kuliwa na wote?
Humu JF kuna members ambao wao tu ni brand kubwa sana, inatisha kuona siku km ya leo wapo kimya, humu kuna wadada wa heshima kubwa kama
Sky Eclat Sakayo Demiss mke wa
Mshana Jr geniveros mumu Jolie Jolie NAHUJA Shunie
JF pia ina majembe yake, brand kubwa tu
Mshana Jr GENTAMYCINE johnthebaptist Tairi bovu Mwifwa Mwana kondoo Quinine korojani IKIRIRI Erythrocyte MTAZAMO MSELA WA MANZESE Ningewataja wote, ila nina kibarua cha kupokea wageni hapa Kijijini kwangu!
On behalf of myself, pamoja nakusikitishwa na ukimya wenu Pasaka hii, nawakaribisha sana mje tujumuike ama laah, muda ndio huu, kwa heshima na taadhima, tumeni wawakilishi wenu, karibuni kwangu, Tubuyu, kama utapata tabu kufika piga simu 26-999, nitapokea mimi!