Hallelujah ya Diamond yaweka rekodi Radio 1Xtra ya UK

Hallelujah ya Diamond yaweka rekodi Radio 1Xtra ya UK

Hongera kwake[emoji106] [emoji106] [emoji106]
 
Ila unaweza kuta iyo radio ni sawa na radio Simiyu tu kwa hapa kwetu.
 
Diamond Platnumz haishi kutuamsha na habari kubwa zinazohusiana na nyimbo zake kila kukicha.

Baada ya kuachia wimbo wake mpya ‘Hallelujah’ ambao amewashirikisha Morgan Heritage kuweka rekodi kubwa ya kufikisha views milioni moja ndani ya masaa 15, wimbo huo umeonekana kufanya vizuri katika kituo cha BBC Radio 1Xtra ya nchini Uingereza.
22279986_130048261077183_1257729895019053056_n.jpg

‘Hallelujah’ umeshika namba moja katika Top 5 ya kipindi cha Afro Boss cha radio hiyo kwa kuzishinda ngoma nyingine kama ‘Inde’ ya Heavy K, ‘Maradona’ ya Niniola, ‘My Baby’ ya Magnom na ‘Nhema’ ya EXQ .

Wimbo huo unaendelea kufanya vizuri nchini humo ikiwemo na kwenye kituo kingine cha Capital Xtra.
Credit - Bongo5

Ushabiki Tanzania unafurahisha sana
 
alianza kunua watamazamaji youtube naona sasa ni radio za dunia
 
Back
Top Bottom