Luhombo Jr
New Member
- Apr 29, 2024
- 1
- 0
Namshukuru Mungu nami kupata nafasi ya kuchangia mawazo yangu katika kuitafuta Tanzania tuitakayo. Maoni yangu yatajikita katika mapinduzi makubwa ya kilimo Kwa maana ya ukulima wa mazao ya mashambani, ufugaji na uvuvi Kwa kuanzisha mfumo wa mashamba vitalu (blok farms) katika Kila halmashauri nchi nzima. Mashamba vitalu haya yataleta mabadiliko makubwa na ya kudumu kutoka katika kilimo Cha kujikongoja (substance farming) Hadi kilimo Cha kibiashara (commercial farming).
Mafanikio ya mashamba vitalu yataleta athari chanya Kwa wakulima wenyewe, viwanda vya bidhaa za kilimo na wafanyabishara Kwa ujumla. Mashamba vitalu haya yatagaiwa. Kwa wakulima na wafugaji wadogo nchi nzima katika mfumo wa mkopo wa masharti nafuu. Yaani Halmashauri itakopesha Kwa wakulima eneo lenye Kila kitu kuhusu kilimo kama miundombinu ya maji Kwa wafugaji na miundombinu ya umwagiliaji Kwa wakulima, mbegu Bora na vitendea kazi pamoja na utaalamu kutoka Kwa mabwana mifugo na mabwana shamba Kwa kipindi chote Cha kulima na kufuga halafu Baada ya kuvuna, halmashauri itasimamia mauzo ya wakulima Hawa wauze bidhaa zao Kwa bei nzuri na baada ya kuuza halmashauri itakata Gharama za uzalishaji ambazo mkulima alipewa kama mkopo afu mkulima atapewa faida iliyobaki kama Pato lake la msimu huo. Halmashauri hazitawakopesha wakulima pesa bali zitawakopesha mashamba na huduma zote zinazohitajika mashambani.
Mashamba yatakuwa yanalima na kuandaa zao la aina Moja Kwa ukubwa mfano kama ni kilimo Cha bustani basi ni bustani tupu na kama kufuga ni aina Moja ya mnyama katika vitalu vyote katika eneo husika. Mashamba haya yatakuwa na huduma zifuatazo.
i/ Eneo la kutosha lenye rutuba
ii/ kutakuwepo na mabwawa au marambo makubwa au mto kama chanzo Cha maji
iii/ kutakuwepo na mifumo ya maji na umwagiliaji eneo lote
iv/ kutakuwepo na miundombinu ya Barabara ndani ya farm bloks na Barabara kuu ya kuunganisha na mji au soko
v/ Kutakuwa na kiwanda Cha kuchakata na kuongeza thamani mazao mfano kama korosho kiwepo walau kiwanda Cha kubangua korosho, na Kama ufugaji Kwa ajili ya maziwa kiwepo kiwanda Cha kuhifadhi maziwa na kuyaongeza thamani
vi/ Kutakuwepo na maghala makubwa kwa ajili ya kuhifadhi mazao Baada ya kuvunwa
vii/ Eneo tengefu La malisho ya wanyama Kwa wafugaji.
ILI KUFIKIA MAPINDUZI MAKUBWA YA KILIMO HALMASHAURI ZIFANYE MAMBO YAFUATAYO KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 5-25 YA UANZISHWAJI WA MASHAMBA VITALU (BLOKS FARMS)
I/ Mtaji wa kwanza wa hii miradi ya mashamba vitalu ni eneo kwa mana ya ardhi. Halmashauri zinatakiwa kuhakikisha maeneo yanapatikana na yanasafishwa vizuri. Maeneo yenye mabonde ya kilimo ndio mazuri zaidi
ii/ Halmashauri zitenge bajeti ya kuendesha hii miradi kupitia mapato ya ndani mfano Kwa kutumia Ile 10% ya vijana walemavu na wanawake. Kupitia hizi bajeti zitawezesha kukodi na kununua mashine za kuchimba mabwawa, za kusafisha maeneo na mashine za kuchonga na kukarabati Barabara ili ziwe zinapitika muda wote ndani ya mashamba na zile za mjini kuja shambani.
iii/ Maji ndo Uti wa mgongo wa mashamba haya hivyo Huduma za maji zipatikane muda wote hasa kipindi Cha kiangazi. Kama hakuna mto karibu visima virefu na mabwawa ya kuhifadhi maji yachimbwe.
iv/ Halmashauri ziajili maafisa kilimo na mifugo na mafundi wa mifumo ya umwagiliaji maalum Kwa ajili ya kuwahudimia wakulima wa eneo husika katika mashamba vitalu yote
v/ Halmashauri zinatakiwa Kuhakikisha vitendea kazi vinakuwepo muda wote kama matrekta na mashine zingine za kilimo
vi/ Masoko mazuri yenye bei nzuri huleta motisha binafsi Kwa wakulima hivyo halmashauri ziwaunganishe wakulima na masoko mazuri ya ndani na nje ya nchi ili kutengeneza faida kubwa. Badala ya kuwatumia madalali wa mtaani kutafuta taarifa za masoko, wanatakiwa wawatumie maafisa biashara na maafisa kilimo wa halmashauri kuwa kiungamishi Cha masoko ya mazao na wakulima kutoka katika miradi hii kwenda Kwa wanunuzi katika halmashauri zao.
vii/ Katika kuongeza ufanisi na maarifa Kwa wakulima ziwepo study tour za mara Kwa mara ndani na nje ya nchi Kwa wakulima wengne wanaofanya kilimo kinachofanana na wakulima ndani ya halmashauri zetu.Hii itasaidia Kuongeza ujuzi wa kutatua changamoto za masoko magonjwa na ubora wa mazao ya kilimo. Mfano sisi tulikuwa na kikundi chetu tulipata bahati ya kwenda Thailand kujifunza kulima muhogo kibiashara
viii/ Kutungwe Sheria ndogo ndogo (by laws) za kusimamia haya mashamba vitalu ili wakulima na halmashauri Kila mtu awajibike ipasavyo katik kuleta matokeo yanayotarajiwa..
BAADA YA KUTEKELEZWA KWA UANZISHWAJI WA MASHAMBA VITALU ( BLOKS FARMS)NDANI YA MIAKA 5-25 IJAYO TANZANIA ITAKUWA IMEPIGA HATUA KAMA IFUATAVYO
I/ Nchi itakuwa na Uhakika wa chakula Cha kutosha Kwa sababu mazao yatakuwa yanalimwa mwaka mzima bila kusubiri msimu wa mvua.
ii/ Nchi itapata fedha za kigeni Kwa kuuza ziada nje ya nchi hasa zile nchi ambazo hazizalishi chakula Kwa wingi mfano mzuri nchi ya Congo wako na machafuko hawana muda wa kuzalisha chakula.
iii/ Tatizo la ajira Kwa vijana litakwisha Kam sio kupungua mana vijana watavutika kuingia kwenye kilimo Kwa sababu kilimo kitakuwa rahisi na sio adhabu.
iv/ Wakulima watainuka kiuchumi na umaskini utaisha kabisa
v/ Halmashauri zitakuwa na uwezo wa kukusanya madeni kirahisi tofauti na Sasa mikopo mingi hailipwi Kwa sababu miradi ya vikundi imekufa
vi/ Viwanda vingi vitaanzshwa nchini Kwa sababu Kutakuwa na Uhakika wa malighafi za kutosha.
CHANGAMOTO ZINAZOWEZA KUKWAMISHA MIRADI HII YA MASHAMBA VITALU
I/ Ufujaji na uharibifu wa miundombinu kama hakutakuwa na elimu ya kutosha Kwa wakulima juu ya utunzaji na utumiaji nzuri wa miundombinu yote ya mradi.
ii/ Mlipuko wa magonjwa na wadudu waharibifu wa mazao kama havitadhibitiwa mapema vitaleta hasara na kuwavunja moyo wakulima.
III/ Mabadiliko ya hali ya hewa hasa kuongezeka Kwa joto au baridi Kali na uwepo wa mvua nyingi kipindi ambacho mvua sio msimu wa mvua
iv/ Sheria na sera za Kodi zisiporekebishwa mazao yatakayozalishwa katika mashamba vitalu vyetu yatakutana na ushindani mkubwa Kwa mazao yanayotoka nje ya nchi hivyo soko litasumbua na kuwakatisha tamaa wakulima.
v/ Mvutano wa wanasiasa hasa katika kuchagua maeneo ya kuanzisha mashamba vitalu usipodhibitiwa utayumbisha na kuchelewesha uanzishwaji wa hii miradi ya mashamba vitalu.
MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUPUNGUZA AU KUZUIA CHANGAMOTO ZITAKAZOKWAMISHA HII MIRADI YA MASHAMBA VITALU KUPITIA MFUMO WA MIKOPO KWA WAKULIMA.
I/ Kuwe na Sheria Kali (by laws) za kusimamia hii miradi ili kudhibiti uharibifu wa miundombinu na Ufujaji wa Mali za miradi.
ii/ Madawa na chanjo zipatikane Kwa muda ili kudhibiti magonjwa ya Mlipuko na magonjwa nyemelezi na kuangamiza kabisa wadudu waharibifu.
iii/ Matumizi ya teknolijia ni muhim Sana katik kukabilian na mabadiliko ya hali ya hewa.Mfano matumizi ya green House nk
iv/ Kuanzia Baraza la madiwani Hadi bunge lazima litunge sera na Sheria za kikodi zitakazo hamasisha mazao yetu kuuzwa nje na mazao ya nje kutoingia nchini ili kulinda soko la ndani.
v/ Wanasiasa kuachana na mivutano isiyo ya lazima katika kupendekeza maeneo ya miradi, pia katika kutenga bajeti na katika vikao vya kimaamuzi.
HITIMISHO
Ukiaangalia nchi nyingi zilizoendelea zilianza na mapinduzi ya kilimo halafu ndo yakaja mapinduzi mengine kama ya Viwanda, teknolijia, kisiasa nk. Hivyo kuiga vitu vizuri sio ujinga na ili watu wengi waingie kwenye kilimo hakitakiwi kilimo kionekane kama adhabu. Kilimo kinatakiwa kionekane kama Binti mrembo anaemvutia Kila kijana aliebarehe.

Upvote
0