Halmashauri kupitisha sheria ya kodi ya mashamba

Halmashauri kupitisha sheria ya kodi ya mashamba

Sema Kweli

Member
Joined
Apr 12, 2013
Posts
53
Reaction score
20
Salaam kwenu wana jukwaa hilii la sheria nimekuja kwenu kwa mara kwanza kabisa nikiomba msaada wenu wa kisheri kuhusu halmashauri inapo pitisha sheria ya kudai kodi kwa wakulima wadogo wa vijijini bila hata kuwashirikisha kwenye mchakato wa uanzishwaji wa kodi husika.

Sina maana hapa kuwa halmashauri wamekosea hapana ila nilidhani kuwa baada ya halmashauri kuja na mapendekezo hayo wange waita wadau wa kilimo na kuwajulisha kusudioo la jambo husika lakini cha kusikitisha ni kwamba hata bila ya kuwajulisha kusudio hilo halmashauri ilicho fanya ni kuwaandiki baadhi ya wakulima barua yenye amri ya kutekeleza ulipaji wa kodi husika kwa muda wa siku saba kwa hiyari na maada ya hapo kitako fuata ni adhabu.

Hoja yangu ninayo taka msaada kwenu iko kwenye vipengele vifuatavyo.

1. Ikumbukwe kwamba mashamba yanayo tajwa hapo halmashauri haiku yapima kwa maana hawana uhakika kama una miliki ama lah kwani nikilinganisha idadi ya watu walio pata barua hizo ni wachache sana sijajua maana yake ni nini.

2. Nijuavyo mimi ni kwamba mahakama pekee ndiyo inayo weza kutoa amri na ina toa baada ya kusikiliza pande husika,sasa hapa sijajua halmashauri imetumia kigezo gani kutoa amri kwa watu ambao hukuwashirikisha kwenye jambo husika.

3. Kodi iliyo pendekezwa nina hisi kuwa ni kodi kubwa sana kwani wameleta amri ya kila mwenye shamba la kuanzia 50 eka atalipia sh 200,000 kwa mwaka,sijui kwa wawekezaji wakubwa wanalipia kiasi gani kwa eka ila nadhani kuwa hawalipi kiwango kikubwa kama hiki.

4. Kwa uelewa wangu nilidhani kuwa afisa biashara angeweza kukutana na wakulima sokoni na sio shambani kwani shambani utakuwa unatoza kodi kitu ambacho sio halisi kwani mkulima atakuwa bado hajavuna na hivyo asipo vuna atakuwa amelipia asicho kipata.

Yawezekana nikawa sijawapangia hoja zangu vizuri ila ni matumaini yangu kuwa kwa kiasi fulani mtaweza kutusaidia sisi wakulima wa vijijini kwani wakati mwingi tumekuwa tukikandamizwa pasipo kujua.
 
Back
Top Bottom