Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es salaam imemteua Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya na Mwanachama wa Chama hicho, Nurdin Bilal Juma (Shetta) kugombea Udiwani Kata ya Mchikichini Wilaya ya Ilala
Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Ally Bananga, ametangaza uteuzi huo leo August 14, baada ya kukamilika kwa Mchakato wa Kura za maoni
Itakumbukwa katika Mchakato wa kura za maoni uliofanyika August 04,2025 ukihusisha Wagombea mbalimbali, Shetta aliwazidi Wapinzani wake kwa kupata jumla ya kura 293 ambapo Azimkhan Akber Azmkhan akipata kura 178 na Joseph John Ngowa akipata kura 7 pekee