Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM yawaita ili kuwahoji Kinana, Makamba na Membe

Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM yawaita ili kuwahoji Kinana, Makamba na Membe

Lazima wajibu tuhuma, CCM kuna demokrasia aise, lazima waende ama sivyo watupwe kule...
 
What goes around comes around. Kwa mila zetu za Kiafrika, wazee hupewa heshima,tusifukue makaburi.
cheusimangala_ umeleta sintofahamu kwenye chama dume.
 
Kazi ngumu sana kwa membe!hapa nayaona mambo mawili!
1:Aende kisha baada ya mazungumzo watoe clip za kumlisha maneno ya kumdhalilisha!!!!ili apoteze heshima na mvuto wa kisiasa!!!
2:Asiende aonekane mtovu wa nidhamu avuliwe uanachama!!!kazi kweli kweli!!!!
 
Heshima ya nchi lazima irudi tujenge nchi yetu sote pamoja bila makundi wala ubaguzi. Hatuwezi kubembelezana na mtu yeyote awe wa CCM au Upinzani, tufike mahali tukubaliane wote kwa pamoja kufuata sheria ambazo tumejiwekea. Kuheshimu mamlaka bila kuvunja sheria nk. angalia UK wapiga kura wamewaadhibu wote waliokuwa wanabeza Brexit na leo hii Theresa May analia uchungu mkubwa maana Boris ameshinda kwa kishindo. Sio kwamba British tax payers wanamkubali sana bali kupeleka message kwamba wapiga kura ndio waamuzi wa kila jambo Serikalini.

JPM kama hafanyi kazi alizopewa na wapiga kura wake ataadhibiwa kwenye box la kura na wala sio majungu ya kwenye mitandao na mavikundi ambayo yalifikiri Tanzania ni yao pekee. Tusisahau makundi makundi hasa wakati wa JMK.
Usilinganishe TZ na UK mkuu kule kura ni huru, ukiona mtu kashindwa basi kashindwa kweli hapa kwetu mnatumia bunduki tu. Eti ataadhibiwa kwa box la kura watu wengine buana!! wakati mtu akionyesha nia ya kutaka kugombea uraisi kupitia CCM anafanyiwa figisu kama hizo ya kudukuliwa na kuitwa kwenye kamati ya maadili halafu ETI ataadhibiwa kwa box la kura? Mkiruhusu demokrasia na kuwaachia wananchi kuamua kweli Jiwe anaweza kuhukumiwa kwa box la kura ila kwasasa TZ wenye maamuzi ni Jeshi, TISS, mahakama, Spika na Msajili wa vyama vya siasa, kwa kupokea amri kutoka kwa Amiri Jeshi mkuu. WANANCHI HATUNA MAAMUZI.
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] Tibaigana Alfred alijiunga lini nae? Maana alionba nafasi ga kugombea ubunge jimbo la Tibaijuka Kajumulo, akapigwa chini. La muhimh tuzingatie kwamba viongozi almost wote waandamizi wa serikali ni pro CCM
Hivi hiyo Zelothe Stephen amejiunga lini na chama cha mapinduzi ?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heshima ya nchi lazima irudi tujenge nchi yetu sote pamoja bila makundi wala ubaguzi. Hatuwezi kubembelezana na mtu yeyote awe wa CCM au Upinzani, tufike mahali tukubaliane wote kwa pamoja kufuata sheria ambazo tumejiwekea. Kuheshimu mamlaka bila kuvunja sheria nk. angalia UK wapiga kura wamewaadhibu wote waliokuwa wanabeza Brexit na leo hii Theresa May analia uchungu mkubwa maana Boris ameshinda kwa kishindo. Sio kwamba British tax payers wanamkubali sana bali kupeleka message kwamba wapiga kura ndio waamuzi wa kila jambo Serikalini.

JPM kama hafanyi kazi alizopewa na wapiga kura wake ataadhibiwa kwenye box la kura na wala sio majungu ya kwenye mitandao na mavikundi ambayo yalifikiri Tanzania ni yao pekee. Tusisahau makundi makundi hasa wakati wa JMK.
Usilinganishe TZ na UK mkuu kule kura ni huru, ukiona mtu kashindwa basi kashindwa kweli hapa kwetu mnatumia bunduki tu. Eti ataadhibiwa kwa box la kura watu wengine buana!! wakati mtu akionyesha nia ya kutaka kugombea uraisi kupitia CCM anafanyiwa figisu kama hizo ya kudukuliwa na kuitwa kwenye kamati ya maadili halafu ETI ataadhibiwa kwa box la kura? Mkiruhusu demokrasia na kuwaachia wananchi kuamua kweli Jiwe anaweza kuhukumiwa kwa box la kura ila kwasasa TZ wenye maamuzi ni Jeshi, TISS, mahakama, Spika na Msajili wa vyama vya siasa, kwa kupokea amri kutoka kwa Amiri Jeshi mkuu. WANANCHI HATUNA MAAMUZI.
 
Watoto wao watakula wapi wewe watenda tu.. Hii ni km familia issue tu
Mzee Makamba na Kinana msiitikie wito huo wa ajabu ajabu unaolenga kuwadhalilisha zaidi baada ya kutendewa unyama wote ule wa kudhalilishwa na Musiba na pia kudukuliwa maongezi yenu private kinyume cha sheria za faragha.
Wazee msikubali kata kata washauri watakoutumwa pembeni yenu kujifanya wanakuja kwa busara ili kuwabembeleza na kuwasihi mwende.

Huyo aliyemtuma Musiba kuwavunjia heshima mbele ya Jamii anataka awatumie nyinyi wenyewe kujisafisha kwa siasa zake zake za kuumiza wenzie.

Nyie makanali wa Jeshi na watumishi wa CCM, hamuwezi kudhalilishwa namna hii na nyie mkaenda kupiga magoti.
KUBALINI MFE KWA HESHIMA, VIZAZI VITAWAKUMBUKA, MSIENDE KUPIGA MAGOTI

Membe Kama una nia ya kugombea uraisi kupitia CCM wewe nenda kawasikilize, kama huna nia ya kugombea uraisi basi potezea maana wewe ndo umetendewa kosa, umedukuliwa mazungumzo private kabisa kinyume cha haki yako faragha na uhuru wa kutoa maoni kwa mujibu wa nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katibu mkuu mstaafu wa CCM mzee Yusuph Makamba amezoeleka kwa nukuu zake za kwenye Biblia takatifu kila awapo kwenye tukio muhimu.

Sitashangaa kumuona mzee Yusuph au Joseph kama anavyoitwa na wazungu akitimba na Biblia katika kikao cha kamati ya maadili kinachomsubiri. Na sitaona ajabu atakoposhuka na mistari ya kibiblia itakayoonyesha katika wajumbe wale wa kamati ya maadili hakuna hata mmoja mwenye " HAKI" ya kustahili kumnyooshea kidole yeye mzee Makamba.

Kuna wakati mwokozi wetu Yesu aliwakuta wayahudi waliokuwa wanajiandaa kumuua kwa kumpiga mawe mwanamke mzinifu, Yesu akawauliza je ni yupi kati yenu ambaye hajawahi kutenda dhambi?.......wakakimbia wote na kumwachia yule mwanamke UHAI wake.

Binafsi nampongeza sana Rais Magufuli kwa kuwasamehe wale waliotubu kwa kuwa hawakujua ( kiroho) walilokuwa wanalitenda.

Niwatakie Sabato njema.

Maendeleo hayana vyama!
 
Back
Top Bottom