Halmashauri Mkalama: Watumishi wanathibitishwa kazini baada ya kukidhi vigezo, wale wa 2024 waliothibitishwa ni 142

Halmashauri Mkalama: Watumishi wanathibitishwa kazini baada ya kukidhi vigezo, wale wa 2024 waliothibitishwa ni 142

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mkalama Mei 21_page-0001.jpg
TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI KUHUSU MADAI YA KUTOTHIBITISHWA KAZINI KWA WATUMISHI WA
HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA


Mei 21/2026, Nduguti, Mkalama, Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama inapenda kutoa ufafanuzi kwa umma kuhusu taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zikidai kuwa baadhi ya watumishi, hususan wa kada ya afya walioajiriwa mwaka 2024, hawajathibitishwa kazini hadi sasa.

Alichoandika Mdau bofya hapa ~ Ajira Mpya Halmashauri ya Mkalama DC – Singida hadi mtu aombe mkopo ndio anathibitishwa kazini?

Ndugu wananchi, hakuna mtumishi aliyeajiriwa mwaka 2024 ambaye amekidhi vigezo vya kuthibitishwa kazini na bado hajathibitishwa. Kwa mujibu wa Kanuni ya 14(1) ya Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2022, mtumishi anapaswa kuthibitishwa kazini baada ya kutimiza masharti yaliyowekwa, ikiwemo kutumikia kipindi kisichopungua miezi nane na kisichozidi miezi kumi na miwili tangu tarehe ya kuajiriwa kwake.

Halmashauri imekwishathibitisha kazini watumishi wote 142 walioajiriwa mwaka 2024 baada ya kutimiza vigezo vinavyotakiwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma.

Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama inatoa wito kwa watumishi wote kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa bidii, uadilifu na kwa kuzingatia maadili, sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma.

Aidha, watumishi wanahimizwa kupata taarifa sahihi kupitia mamlaka husika na kuepuka upotoshaji unaoweza kusababisha taharuki isiyo ya lazima.

Seleman S. Musunga
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji (W) Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama
MKURUGENZI MTENDAJI
21 Mei, 2026
 
Back
Top Bottom