KERO Halmashauri wilaya ya kishapu haijawalipa walimu wa sekondari(ajira mpya) pesa ya kujikimu

KERO Halmashauri wilaya ya kishapu haijawalipa walimu wa sekondari(ajira mpya) pesa ya kujikimu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mtu na nusu

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2020
Posts
704
Reaction score
1,381
Kile kilio cha walimu ajira mpya kutokulipwa pesa zao za kujikimu kimeifikia wilaya ya kishapu.

Awali uongozi wa halmashauri ulisema haujalipa kwa sababu pesa haijafika kutoka hazina, ila baada ya tamko la waziri kuwa pesa yote imeshazifikia halmashauri, kishapu iliwalipa walimu wa msingi pekee na kuwaacha walimu wa sekondari.

Ombi langu ni kuwaomba viongozi na wanafamilia wenye connection ambao wako humu, wasaidie ili pesa ya kujikimu iwafikie ajira mpya wote, mambo ni magumu sana ukizingatia ugumu wa mazingira wa hii halmashauri.

Jamiiforum ni familia na humu kuna viongozi wengi nyeti ambao wanaweza kulifatilia hili na kulipatia majibu, msaada wenu ni wa muhimu sana katika kuhakikisha kila mtumishi anapata anachostahili ili aweze kutimiza majukumu yake bila kikwazo.

Asanteni.
 
Back
Top Bottom