Johnson Alex Otieno
Senior Member
- Mar 14, 2013
- 172
- 57
Salaam wana jukwaa,
Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa uzima na afya njema, pia niwashukuru watumishi wote nchini Tanzania kwa kuendelea kujenga Taifa letu bila kujali kadhia mnazokumbana nazo toka kwa wakuu wenu wa vitengo na wengine wengi waliopewa mamlaka ya kusimamia maslahi na haki zenu.
Nijikite kwenye mada, Kwa wa sio fahamu Bukombe ni moja ya wilaya za Mkoa wa Geita.
Ndani ya halmashauri ya Bukombe kuna mambo mengi yanayokatisha tamaa na shauku ya watumishi kufanya kazi kwa bidii na kutumia talanta/vipaji vyako kikamilifu.
Mambo hayo ni kama yafutayo:
1). Kucheleweshwa kwa malipo ya uhamisho na wakati mwingine kutokulipwa kabisa.
Imekuwa ni kawaida kwa watumishi wa kada ya elimu(walimu) kuhamishwa bila kufata taratibu na kanuni za kazi.
Mfano mwezi Machi shule nyingi mpya zimefunguliwa na walimu walihamishwa toka eneo moja la kazi na kupelekwa km nyingi bila kukamilisha malipo yao.
Jambo hili limeathiri utendaji wao, kwa ni huko walikopelekwa hakuna nyumba za watumishi hivyo watumishi hawa walazimika kusafiri umbali mrefu ili kutimiza takwa la kazi.
Naomba wakuu walipeni watumishi fedha za uhamisho mapema ili wapate unafuu wa maisha na wakidhi gharama za nauli, mathalani mwalimu mmoja hutumia elfu tano kwa siku ili kufika kituo cha kazi, wengine huendesha baiskeli kwa zaidi ya km 36 kwa siku kwenda kituo chake cha kazi kwa kazi.
Ifike wakati jibu la mchakato unaendelea lisitamkwe.
Wapeni fedha ili wafanye kazi, uhamisho sio adhabu.
2) Fedha za kujikimu kwa watumishi wapya/ajira mpya.
Imekuwa ni kawaida kwa halmashauri ya bukombe kuchelewesha fedha za kujikimu kwa watumishi wapya, hali hii imefanya watumishi wengi washindwe kufanya kazi kwa ufanisi na kufikia lengo.
Mara nyingi halmashauri inasubiri watumishi wafike ofisi ya mkurugenzi kumsumbua kwa kushinikiza malipo yao, nje ya utaratibu wa kushinikiza malipo yao, majibu huwa mchakato unaendelea na kuambiwa barua zimekosewa.
Kuna maelekezo mengine, punguzeni michakato tafadhari. Lipeni watumishi madai yao kwa wakati, watumishi hawa ni binadamu, wana mahitaji na wana familia zinawategemea.
Ijumaa kareem