Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imetoa ufafanuzi kuhusu uendeshaji, utaratibu wa maegesho, pamoja na utozaji wa faini kwa vyombo vya usafiri wa umma, hasa pikipiki za miguu miwili (bodaboda) na miguu mitatu (bajaji), ili kuondoa taharuki na usumbufu kwa madereva pamoja na wananchi.
Akijibu hoja zilizotolewa na Wadau mbalimbali wa JamiiForums.com, kuhusu hoja za kuwa kuna baadhi ya Maafisa wa Jiji wakiwemo Mgambo kukamata Madereva Bodaboda na Bajaj wanaoshusha na kupakia abiria kisha kuwatoza faini ya Tsh. 50,000 kwa kosa la kuegesha maeneo yasiyo stahili (wrong parking), Meneja wa Maegesho wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Neema Ngavatula anafafanua:
Halmashauri pamoja na Kamati iliyoundwa na Mkuu wa Wilaya na Uongozi wa Halmashauri imetenga na kusajili vituo maalum kwa ajili ya bodaboda na bajaji wanaofanya shughuli zao katikati ya jiji.
Hatua hiyo imechukuliwa ili kudhibiti tabia ya baadhi ya madereva kupaki kwa fujo (zig-zag) katika maeneo yasiyoruhusiwa, hususan kwenye vituo na njia za mabasi ya mwendokasi mfano eneo la Msimbazi Kariakoo.
Wengine wanaegesha mbele ya mitaa ya maduka, vituo vya polisi, na maeneo ya hifadhi ya barabara yanayosababisha kero na msongamano wa magari.
Kuhusu Madereva wa Mtandao, Halmashauri haimkamati dereva anayeshusha au kupakia abiria, kwani kitendo hicho huchukua muda mfupi (dakika moja au mbili).
Anayekamatwa ni yule tu anayeegesha eneo ambalo halitakiwi, tumeshaweka utaratibu kuwa Madereva wa Mtandao wanaosubiri maombi ya abiria wametengewa maeneo rasmi yakiwemo Uwanja wa Mnazi Mmoja, maegesho ya Shule za Msingi, Kariakoo Sokoni, na Machinga Complex.
Dereva anapopata simu au ombi la abiria, anaruhusiwa kwenda kumfuata hapo alipo, kumpakia ndani ya dakika moja, na kuondoka bila kuegesha gari au pikipiki yake pembezoni mwa barabara zilizokatazwa.
Tumeshaelekeza maafisa wetu kuwa hawatakiwi na wanafahamu kuwa sisi hatukamati wale wanaochukua abiria au wanaoshusha bali ni wale wanaoegesha kabisa maeneo yasiyo stahiki.
Kwa dereva yeyote anayekiuka sheria na kuegesha chombo chake katika eneo lisiloruhusiwa Faini ni Shilingi 50,000, ikiwa chombo chake kitabebwa na faini inaongezeka kuwa Sh 70,000.
Faini zote zinalipwa kwa Namba ya Malipo (Control Number) au mashine za kielektroniki (POS) zinazotoa risiti halali za mashine hakuna malipo ya fedha taslimu yanayoruhusiwa mkononi.
Natoa rai kwa madereva wote wa bodaboda na bajaji ambao bado hawajapata utaratibu au vituo rasmi kufika katika Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuanzia Saa 1:00 Asubuhi hadi Saa 12:00 Jioni, Jumatatu hadi Jumamosi watapata maelekezo, watajisajili na ambao hawana vituo watapangiwa.
Soma pia kuhusu

- Walinzi wa Halmashauri wanakamata Pikipiki Kariakoo kwa kuita "wrong parking" bila utaratibu
- Mgambo Kariakoo wanatumia kigezo cha 'faini' kuomba rushwa kwa Bodaboda na Bajaj
- Hivi Mgambo wa jiji hapa Dar ususani Ilala wana nguvu kuliko Waziri Mkuu?
- Huyu ni moja ya waliojitambulisha kuwa Askari, anasumbua sana Bodaboda na Bajaj mitaa ya Kariakoo
- Halmashauri ya Jiji la Dar yasitisha ada ya maegesho Mjini
- Maafisa usafirishaji wa mtandao, maarufu kama bodaboda za mtandao, wamefunga barabara katika eneo la Chuo cha Biashara (CBE) Posta - Dar
- Kuna rushwa kubwa na utaratibu usiofuatwa katika ukamataji wa Bajaj na Bodaboda
- Mgambo wanaotoza bodaboda na Bajaj faini ya Tsh. 50,000 kila siku wanatutengenezea chuki Wananchi
- Mgambo na Trafiki wananyanyasa watu Kariakoo, ndio maana Rushwa haiishi!