Halmashauri ya Jiji la Arusha kuimiliki AFC

Halmashauri ya Jiji la Arusha kuimiliki AFC

Jackbauer

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Posts
6,053
Reaction score
2,207
Halmashauri ya jiji la Arusha chini ya mkurugenzi mpya imeamua kuichukua timu ya AFC ambayo kwa sasa iko ligi daraja la pili.Manispaa ya jiji imeamua kuichukua timu hiyo iliyokuwa ikiwakilisha Arusha katika ramani ya michezo au mpira wa miguu kwa miaka mingi kabla ya kufulia.

Inasemekana hili ni wazo la mkurugenzi mpya wa jiji ambaye ana historia ya kuiibua timu ya Mbeya city alipokuwa mkurugenzi wa manispaa ya mbeya.

kwa sasa AFC itajulikana kama ACFC ...ARUSHA CITY FOOTBAL CLUB!

Kila la kheri mkurugenzi.

=====================
=====================

juma-iddi.jpg

Mkurugenzi wa jiji la Arusha, Juma Iddi (mwenye suti nyeusi).


Mkurugenzi wa jiji la Arusha, Juma Iddi amepania kuipandisha ligi timu ya Arusha FC inayoshiriki ligi daraja la pili msimu huu, huku akiwataka viongozi wa sasa wa timu hiyo kuwa kama kamati na jiji hilo kuhakikisha swala hilo linafanikiwa.


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mapema ofisini kwake alisema kuwa kwa kuwa tayari usajili umekwisha fanyika kwa sasa wanatafuta kocha mwenye ujuzi na uwezo wa kimataifa wa kuwanoa vijana hao ili kuweza kumudu mikiki ya ligi daraja la pili bila kuwa na woga.


"Kiukweli mimi napenda michezo na niko hapa halmashauri ambapo kazi kubwa ni pamoja na kuitangaza michezo na kuonyesha mfano hivyo kwa kuanzia tumeipa nguvu ya kushiriki michuano hiyo kwa vifaa vyote walivyohitaji vya michezo lengo wasianze kulalama na vifaa".


"Na baada ya vifaa sasa tutahakikisha inakuwa mikononi mwetu mapema mwezi ujao baraza la madiwani litakapokaa na kuridhia na baadhi ya watendaji wa halmashauri hii watakuwa miongozi mwa viongozi watakaochaguliwa kuiongoza lengo ni kuileta karibu na kujua mahitaji yao" alisema Juma Iddi.


Alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi wa Arusha kuhakikisha wanakuwa karibu zaidi na timu hiyo na ilete chachu ya soka mkoani hapa kwa kuishangilia na mawazo pia maoni yao.


"Sisi kama halmashauri kuimiliki timu hii siyo kuwaweka mbali wananchi bali ni kuweza kuwajulisha kuwa pia kuwa timu hiyo ni yao kwani itakuwa inatangaza jiji pia kodi zao ndio zitatumika na wajue kuwa pia hatutachukua moja kwa moja bali kwa mda ili tu kuipandisha"


Alitumia fursa hiyo kuwataka mashabiki wa soka wa mkoani hapa pamoja na benchi la ufundi na wachezaji kuwa kitu kimoja na wasiruhusu migogoro kati yao kwani kufanya hivyo kutakatisha matumaini ya kupanda ligi bali wawe kitu kimoja kuhakikisha lengo linafanikiwa.

DewjiBlog
 
thats good ideal atapata support kubwa ya wanaarusha
 
Wameanza kwa kuinunulia vifaa vya milioni nne.
 
Kila la kheri ACFC katika mbio zenu za kupanda ligi kuu.
 
Timu inayopewa support ndio inakuwa nzuri. Tunategemea timu yenye ushindani kutoka Arusha ili kuinua soka la Tanzania
 
Arusha haina historia nzuri ya soka...

Nina wasiwasi support itakuwa ndogo na hatimaye kusiwe na mafanikio yoyote...
 
There is no way AFC inaweza kusaidika.

Uongozi umejaa watoto wakiswahili wasiokuwa na fikra endelevu. Wanaganga njaa na kumpinga kila anayekuja na wazo jipya. Kutwa kucha ni majungu, fitina na kukesha kuchanja mrungi

Mkurugenzi asipokuwa makini atajiabisha
 
There is no way AFC inaweza kusaidika.

Uongozi umejaa watoto wakiswahili wasiokuwa na fikra endelevu. Wanaganga njaa na kumpinga kila anayekuja na wazo jipya. Kutwa kucha ni majungu, fitina na kukesha kuchanja mrungi

Mkurugenzi asipokuwa makini atajiabisha


Pumbavu!!! Wewe ungejua watoto wa Kiswahili ndo wanaibeba AFC usingeongea maaluni mkubwa wewe!! Timu inakuaga na Hali mbaya tunachangia hata msosi wa wachezaji... Hawaitegemei AFC , Bali timu inawategemea wao.
Sijui hujui au unajitoa UFAHAMU! Wanaouwa AFC ni Gerald na wambulu wenzake utukome! AFC hata huko daraja la pili anambwela!! Sisi tunataka timu ya kutuburudisha tukikachanja gomba FYI JKT Oljoro anapanda burudani pale pale na Leo karibu Ground UONE Toto anavyokalia dushelele!! Usihofu ntakupa rubesa mbili na wewe uchanje
 
Arusha haina historia nzuri ya soka...

Nina wasiwasi support itakuwa ndogo na hatimaye kusiwe na mafanikio yoyote...

Mzee unaijua AFC, zamani Ndovu Simba na Yanga wanatujua, Mtibwa ashapigwa 5 pale Amri Abeid!! Unawajua wazee wa MOJA MOJA! Bangi Bao?? Karibu Sheikh Amri Abeid....
 
Back
Top Bottom