humphrey_on_th_forum
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 278
- 233
safi yangefanyika nchi nzimaView attachment 735150
Halmashauri ya jiji la Arusha imeaanda maandamano makubwa ya michezo ambayo yatafanyika siku ya sherehe ya maadhimisho muungano April 26, 2018 jijini Arusha
Afisa michezo wa jiji la Arusha, Benson Maneno amethibitisha hilo na kusema kuwa maandamano hayo yatafanyika asubuhi kuelekea katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume ambapo ndipo zitafanyika fainali za michuano ya Muungano Cup na kumpata mshindi wa michuano hiyo, ambapo mshindi wa kwanza atapata milioni mbili, mshindi wa pili milioni moja na mshindi wa tatu laki tano.
"Mashindano hayo ambayo yameanzishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa jiji la Arusha akishilikiana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Dakalo wameanzisha mashindano haya maalum kwa kata zote 25 ambapo watashirikisha vijana wenye umri chini ya miaka 26, hivyo kila kata itacheza na kata nyingine ili kupata mshindi wa michuano hiyo.
Fainali hizo zitafanyika jioni lakini asubuhi ya tarehe 26 kutakuwa na maandamano makubwa ya wana michezo kuelekea uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume kwa ajili ya kufanya fainali hiyo ya Muungano CUP" alisema Benson Maneno
Lakini kwa upande mwingine, siku hiyo hiyo ya Muungano 26 April, 2018 watu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii wakiongozwa na mwanaharakati wa mitandao Mange Kimambi pia wamepanga kufanya maandamano ya nchi nzima kupinga baadhi ya vitu ambavyo vinaendelea nchini kwa sasa.
Chanzo: EATV
Eti mimi Jiwe!!Aibu kwa Chadema wanaomkumbatia Mange!
Narudia:Promo ya bure kwa yale mengine yaleeeeee. Amina Mungu amejibu maombi kwamba maand&&&@@.oooo ruksa Hivi wanaelewa matokeo ya hii kitu? Hahahhh wajinga ndio waliwao
Wakati wao wanaelekea uwanjani sisi tutakua tunaelekea CLOCK TOWER kuadhimisha muungano vizuri.Aliyegundua huu mpango nampa pongezi.kafikiria sana.mabango ndo yatatutofautisha.
kama ni kweli kabla jogoo hajawika simu kutoka juu litakuwa limeshatua Arusha kwa GamboView attachment 735150