KERO Halmashauri ya Jiji la Mbeya rekebisheni mitaro ya maji maeneo ya Kabwe

KERO Halmashauri ya Jiji la Mbeya rekebisheni mitaro ya maji maeneo ya Kabwe

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mwanongwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2023
Posts
879
Reaction score
814
Habari ndugu zangu, ndugu yenu Mwanongwa katika pitapita zangu leo nimeibukia maeneo ya Kabwe Jijini Mbeya.

Kuna mitaro maeneo ya Kabwe njia ya kwenda Block T ni janga kubwa sababu maji na inaleta kero kubwa kwa vyombo vya usafiri hii ni kutokana na maji hayo kuharibu barabara. Mitaro hiyo imekuwa ikimwaga maji barabarani na kusababisha uchafu kutapakaa mtaani.

Kibaya zaidi ni kwamba mvua ikinyesha na maji kujaa, hali ya mitaro kutema maji kusambaa mtaani au barabarani inaweza kubaki hivyo kwa siku kadhaa hadi wiki, hii ni hatari kwa usalama wa afya.

Ombi kwa wahusika kurekebisha mitaro hiyo kwa kuweka makaravati makubwa ili kuruhusu maji kupita kwa urahisi kipindi hiki cha masika.

Tunaomba lifanyiwe kazi hili jambo kabla ya maafa na magonjwa ya mlipuko kutokea.

Ni hayo tu ndugu zangu,
DSC_1432.JPG
DSC_1427.JPG
DSC_1424.JPG
DSC_1429.JPG
 
Hiyo mbeya ni ya hivo hivo siku zote. Nafkri katika majiji machafu hapa Tz inaweza kuwa nafasi ya pili ikitanguliwa na DSM.
 
Mipango miji ni muhimu sana.
Mikoa kama mbeya, iringa,rukwa, ilipaswa kuwa ni kilimo, ufugaji , uvuvi , viwanda vya chakula, akiba cha chakula kwa Taifa, mbolea.

Haikupaswa kuwa na shughuli za kawaida za serikali.
 
Back
Top Bottom