Wiki iliyopita tuliwasilisha ujumbe wetu hapa JamiiForums tukiitaka TAMISEMI na Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, kutufanyia mpango wa fedha zetu za kujikimu, barua ya TAMISEMI ya tarehe 04/06/2026 ilizitaka Halmashauri kuhakikisha watumishi wapya wa afya wanalipwa na kuwasilisha taarifa za utekelezaji ifikapo tarehe 15/06/2026.
Napenda kutoa mrejesho kuwa tumelipwa, uungwana ni busara, kama tulilalamika hapa na ni bora tuweke wazi hapa pia.