KERO Halmashauri ya Mbomba - Songwe ajira mpya Kada ya Afya tumelipwa pungufu fedha za kujikimu

KERO Halmashauri ya Mbomba - Songwe ajira mpya Kada ya Afya tumelipwa pungufu fedha za kujikimu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mtumishi Halmashauri ya Mbomba mkoa wa Songwe ajira mpya Kada ya Afya tunadai pesa zetu za kujikimu kwa muda mrefu sana sasa, Julai 12, 2026 wamelipa ila wamelipa pungufu wakati walisema kuwa serika imeshaingiza pesa zote hivyo tutalipwa zote bila ubaguzi.

Ajabu wamelipa kiwango tofauti tofauti japo kuwa kiwango cha elimu ni sawa tumefuatilia wanadai kuwa ni mwongozo upo, lakini wilaya zingine nyingi hata wilaya ambazo zipo ndani ya huu mkoa wamelipwa laki 9 na kuendelea wilaya yetu wametoa, wengine laki 6 na wachanchi ambao wapo hospitali ya wilaya wamelipwa milioni.
 
Hili swala la pesa za kujikimu serikali ichunguze kuna harufu ya upigaji.
 
Back
Top Bottom