Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia Halmashauri ya Mji Kibaha iliyopo Mkoani Pwani kupandishwa hadhi na kuwa Manispaa.
Uamuzi huo umetangazwa leo Januari 27 na Waziri wa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa wakati akizungumza katika mkutano wa CCM uliofanyika Januari 27 katika viwanja vya stendi ya zamani Mailimoja Kibaha Mkoani Pwani.
Soma Pia: Mohammed Mchengerwa: Rais Samia Ameipandisha Hadhi Geita kuwa Manispaa na Rufiji kuwa Halmashauri ya Mji
Mchengerwa, ametangaza hilo wakati akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na Wananchi katika mkutano mkubwa wa kuunga mkono maazimio ya mkutano Mkuu wa CCM Taifa uliomteua Rais Samia kuwa mgombea wa Urais mwaka 2025.