KERO Halmashauri ya Mkalama-SINGIDA, walimu ajira mpya 2026 hatujalipwa pesa zetu za kujikimu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Walimu ajira Mpya halmashauri ya Wilaya Ya MKALAMA-SINGIDA hatujalipwa Pesa zetu za Kujikimu Tangu Tumeripoti mwezi January 2026.

Kila tukifuatilia Tumekuwa Tukipewa Majibu yasioridhisha kwetu sisi. Kwani Pesa ya Kujikimu kwa mtumishi wa Ajira mpya ni Haki kisheria. Hii inapelekea matatizo ya afya ya akili na kupunguza motisha ya utendaji kazi kwetu sisi Kulingana na Mazingira ya Kazi Kuwa ni Magumu (Makazi kwa watumishi).

Tunaomba Jamii Forum itusaidie kutupazia Sauti kwenda Mamlaka husika @Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, Juu ya hii Kero yetu sisi kama watumishi wa Ajira mpya.

FSrpBqbWQAA5N9K.jpg
 
Sisi ni walimu wa ajira mpya halmashauri ya mkalama 2026. Hadi sasa tumekuwa tukifuatilia madai ya malipo yetu ya pesa za kujikimu bila mafanikio yoyote na majibu yoyote ya kueleweka kutoka kwa wahusika.

Tunaomba halmashauri husika itupatie malipo yetu ya fedha za kujikimu kwani ni haki kisheria inabidi yalipwe ndani ya siku 14 tangu tarehe ya ajira sasa ni miezi mitano bila malipo hayo kwani inapelekea kuwa na mwanzo mgumu wa kazi na kutukatisha tamaa kabisa.

Tunaomba mtusaidie kupaza sauti yetu sisi kama wadau wa JF
 
Sisi ni Walimu Ajira Mpya Halmashauri Ya wilaya ya Mkalama Mkoa wa Singida tumekuwa tukidai malipo ya fedha za Kujikimu tangia tumekuja kuripoti mwezi January, 2026 Hadi sasa bado atujapata malipo ayo ambapo inapeleka kuishi maisha magum ya kazi na kushusha morali ya utendaji kazi wetu kuwatumikia wananchi, Tunaomba mamlaka usika itumulikie hili tulipwe stahiki zetu tuchape kazi kwa moyo mmoja kuijenga nchi yetu.
 
Ajira mpya mnadeka sana ujue, tangia january maana yake tayari unapata mshahara . Tumia mshahara pesa yenu ya kujikimu ikipatikana mtalipwa
 
Hivi kwanini malalamiko ni ya walimu, na kada ya Afya
Sijawahi kusikia wahasibu, Wachumi, ma engineers wakilalamika kuhusu fedha za kujikimu??
 
Halmashauri ya wilaya ya Butiama
Kaimu Mkuu wa idara ya ujenzi ananyanyasa wafanyakazi wenzie kwa maneno chonganisi.

Nilikuwa na matatizo ya kifamilia nimeomba ruhusa kwenye mfumo, lakini nakuja kupigiwa simu na kaimu Mkuu wa idara ya ujenzi kuwa ameulizwa na mkurugenzi niko wapi, majibu yake ni kwamba hatambui niko wapi Ananisukuma kwa maneno nikajieleze mwenyewe.

Serikali wekeni utaratibu mzuri kwa wafanyakazi, Kwa maelezo haya naomba nihame Halmashauri kwani siwezi fanya kazi na mbaya wangu ofisi moja.
 
hatari hahahhhahah
 
Sisi ni walimu wa ajira mpya wa mwaka 2026 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama. Tangu tulipoanza kazi tumekuwa tukidai malipo ya fedha zetu za kujikimu, ambazo kwa mujibu wa taratibu za Serikali zinapaswa kulipwa ndani ya siku saba baada ya kuripoti kazini.

Hata hivyo, hadi sasa imepita takribani miezi sita bila kupokea stahiki hizo. Kinachotuumiza zaidi ni kwamba wenzetu wa kada ya afya katika halmashauri hiyo tayari wamelipwa sehemu ya fedha zao, huku sisi walimu tukiachwa katika sintofahamu bila taarifa yoyote kuhusu lini tutalipwa.

Kutokana na hali hii, tumekuwa tukifanya kazi katika mazingira magumu tangu mwanzo wa ajira zetu, huku tukikabiliwa na changamoto za kujikimu na kutekeleza majukumu yetu ipasavyo.

Tunaiomba JamiiForums na wadau wengine kutupazia sauti ili malalamiko yetu yawafikie wahusika, hususan mamlaka zinazohusika na malipo ya watumishi wa umma. Tunaomba stahiki zetu zilipwe kwa wakati ili tuweze kutekeleza majukumu yetu kwa utulivu na ufanisi.
 
umepelekwa kwenye wilaya nzuri yenye fursa kibao ila bado unalalamika..Msimu wa mvua ukifika ingia mashambani ulime mahindi,alizeti,karanga, dengu na vitunguu.
 
Pesazenu tutawaingizia ila sio kwa muda mnaoutaka nyinyi...Subirini mwaka mmoja na nusu upite ndipo mtaona mshahara ume double kwenye accounts zenu za benki.

Kawaambie na wenzako.
 
Sisi ni walimu wa ajira mpya katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, walioajiriwa mwezi Januari 2026. Hadi sasa tumefikisha takribani miezi saba bila kulipwa stahiki zetu na mamlaka husika haijatoa ufafanuzi wa lini tutalipwa.

Hali hii imeshusha morali na motisha ya kufanya kazi, kwani tunakabiliwa na changamoto za kujikimu katika maisha ya kila siku. Tunaomba mamlaka husika isikie kilio chetu na kusaidia kufikisha suala hili ili stahiki zetu zilipwe kwa wakati.

Ni haki ya kila mtumishi, hasa mwajiriwa mpya anayeanza safari yake ya kazi, kupata malipo na stahiki zinazomstahili ili aweze kumudu gharama za maisha na kujiweka katika mazingira bora ya kutekeleza majukumu yake.
 
Hili
Walimu ajira Mpya halmashauri ya Wilaya Ya MKALAMA-SINGIDA hatujalipwa Pesa zetu za Kujikimu Tangu Tumeripoti mwezi January 2026.

Kila tukifuatilia Tumekuwa Tukipewa Majibu yasioridhisha kwetu sisi. Kwani Pesa ya Kujikimu kwa mtumishi wa Ajira mpya ni Haki kisheria. Hii inapelekea matatizo ya afya ya akili na kupunguza motisha ya utendaji kazi kwetu sisi Kulingana na Mazingira ya Kazi Kuwa ni Magumu (Makazi kwa watumishi).

Tunaomba Jamii Forum itusaidie kutupazia Sauti kwenda Mamlaka husika @Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, Juu ya hii Kero yetu sisi kama watumishi wa Ajira mpya.

View attachment 3585395
Hili tatizo limekuwa kero sana kwa muda mrefu sasa. Ni heri serikali iweke utaratibu mpya. Nini kinashindikana kupangilia mambo sawa. Unakuta mchakato wa ajira unachukua karibia mwaka tangu nafasi zinatangazwa, huwa wanakwama wapi kuseti mahesabu yao muda wote huo. Sasa nafasi inatangazwa miezi nane yote wanasubili kuitwa interview, nikafikiri huwa wanaweka mambo yao sawa!
 
Halmashauri ya wilaya ya Butiama
Kaimu Mkuu wa idara ya ujenzi ananyanyasa wafanyakazi wenzie kwa maneno chonganisi.

Nilikuwa na matatizo ya kifamilia nimeomba ruhusa kwenye mfumo, lakini nakuja kupigiwa simu na kaimu Mkuu wa idara ya ujenzi kuwa ameulizwa na mkurugenzi niko wapi, majibu yake ni kwamba hatambui niko wapi Ananisukuma kwa maneno nikajieleze mwenyewe.

Serikali wekeni utaratibu mzuri kwa wafanyakazi, Kwa maelezo haya naomba nihame Halmashauri kwani siwezi fanya kazi na mbaya wangu ofisi moja.
Hiyo ruhusa kwenye mfumo ilikubaliwa?.Je, hapo panashida.
 
Back
Top Bottom