KERO Halmashauri ya Nachingwea inalazimisha wafanyakazi kuchangia sherehe za mwenge wa uhuru

KERO Halmashauri ya Nachingwea inalazimisha wafanyakazi kuchangia sherehe za mwenge wa uhuru

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Halmashauri ya Nachingwea mkoa wa Lindi kuna kero ya kulazimishana michango ya mbio za mwenge kila mfanyakazi anatakiwa kuchangia Tsh 10,000/=

Hii ni lazima siyo hiari unaitoa wapi utajua mwenyewe kinachotakiwa ni mchango, imefika hatua wafanyakazi wanatishiwa usipotoa unaitwa ukajieleze kwanini hujatoa.

Wakati huo huo mnaambiwa halmashauri imevuka malengo ya ukusanyaji wa mapato.

Hivi inakuwaje mwenge usiwe na bajeti mpaka kuchangishana tena kwa vitisho
 
Back
Top Bottom