Halmashauri ya Nyansa yasema "Vyoo vya Shule ya Msingi Lima kwa sasa vimekarabatiwa na kusafishwa vizuri kwa ajili ya Wanafunzi"

Halmashauri ya Nyansa yasema "Vyoo vya Shule ya Msingi Lima kwa sasa vimekarabatiwa na kusafishwa vizuri kwa ajili ya Wanafunzi"

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Taarifa ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa imeeleza kuwa usafi umefanyika katika vyoo vya Shule ya Msingi Lima baada ya malalamiko kuhusu uchafu na ubora wake:

Taarifa kamili
Kuhusu uchavu wa vyoo na Usafi usioridhisha katika Shule ya Msingi Lima iliyopo Wilaya ya Nyasa kwa sasa vyoo hivyo vimekarabatiwa na kusafishwa vizuri kwa ajili ya Wanafunzi wetu.

Aidha, kwa Bajeti hii ya 2025/2026 kiasi cha Shilingi 82,000,000/- kimetengwa kwa ajili ya Kujenga vyoo matundu 5 na Madarasa 3 kwenye shule hiyo.

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa


WhatsApp Image 2025-08-21 at 17.39.40_a8e57f79.jpg
Pia soma ~ Choo cha Wanafunzi Shule ya Msingi Lima, Wilaya ya Nyasa (Ruvuma) ni kibovu sana na kichafu
 
Serikali ya Samia imeoza kabisa.Yaani Hadi watu walalamike ndiyo wajenge choo Cha shule? Ina maana serikali nzima hawajui wajibu wao?
 
Inatakiwa kuajiri watu wa kufanya usafi kila saa

Huwa nashangaa sana kwanini vyoo huwa havisafishwi kila sehemu
Ukienda Hospital unaondoka na maradhi mengine

Ukienda vyoo vya stendi ndio kabisa
Sasa hizo bajeti za ujenzi huwa hakuna fungu la usafi na maji?

Africa maajabu hayaishi
 
Kujenga choo kimoja kwa Mil 16 bado ni utapeli.
 
Hii ndio serikali ya chura a.k.a Dalali ukilalamika ndio utafikiwa mkikaa kimya imekula kwenu. Ni takataka kabisa kua na mtawala Dalali katika taifa.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom