Halmashauri ya Siha mliwaza nini kumpa barua ya uhamisho mwalimu huku mkijua hakuna hela za kumwezesha kuhama?

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
21,387
Reaction score
44,030
Barua ya uhamisho mlitoa mwezi wa 11 mwaka 2025 halafu malipo ya kwanza Tsh 360,000/= mkatoa Januari 2026. Hivi kabla ya kuandika barua ya uhamisho hamkujua kuwa hakuna hela? Kinachokera zaidi pesa yenyewe mmelipa kwa mafungu karibia mwaka mzima. Na hii inawezekana ubishi wa mwalimu umechangia yeye kupata hizo hela zake japo kwa mafungu.

Mimi ninashauri aliyeandika barua ya uhamisho atumbuliwe kwa sababu kaisababishia serikali hasara ya kulipa mshahara wa bure kwa mwalimu aliyekuwa hafanyi kazi akisubiria hela zake za uhamisho. Ingawa huyu mwalimu naye ni mbishi ila katika hili kafanya vyema kuwagomea hawa miungu watu wanaoonea walimu bila sababu.

Na kama kuna waalimu wamehama bila kulipwa pesa za uhamisho muwaongezee angalau 25% ya hela wanazodai kwa kuwacheleweshea malipo.
FB_IMG_1790080913956.jpg
FB_IMG_1790080905074.jpg
ml
 
Huyo mwalimu pia hapendi kazi yake, kwani hawezi kuhama na fedha zake akaendelea kusubiri akiwa tayari kituo chake kipya cha kazi?
 
MWALIMU OMARI KAWAPELEKEA MOTO LOKO GAVAMENTI MPAKA WAMEKUJA NA UFAFANUZI.
Basi OMARI umelipwa karipoti sasa mkubwa umeeleweka.
 
Kama wanaweza kuhandika barua ya kujiuzuru makamo wa raisi tena barua hiyo inatoka CCM hata kamati ya chama chenyewe nayo empty wanashindwa kwa mwalimu.
 
Barua ya kimkakati hii😅😅😅,halmashauri Wana zengwe sana.
 
Barua ya uhamisho mlitoa mwezi wa 11 mwaka 2025 halafu malipo ya kwanza Tsh 360,000/= mkatoa Januari 2026. Hivi kabla ya kuandika barua ya uhamisho hamkujua kuwa hakuna hela? Kinachokera zaidi pesa yenyewe mmelipa kwa mafungu karibia mwaka mzima. Na hii inawezekana ubishi wa mwalimu umechangia yeye kupata hizo hela zake japo kwa mafungu.

Mimi ninashauri aliyeandika barua ya uhamisho atumbuliwe kwa sababu kaisababishia serikali hasara ya kulipa mshahara wa bure kwa mwalimu aliyekuwa hafanyi kazi akisubiria hela zake za uhamisho. Ingawa huyu mwalimu naye ni mbishi ila katika hili kafanya vyema kuwagomea hawa miungu watu wanaoonea walimu bila sababu.

Na kama kuna waalimu wamehama bila kulipwa pesa za uhamisho muwaongezee angalau 25% ya hela wanazodai kwa kuwacheleweshea malipo.
View attachment 3675748View attachment 3675749ml
Maelezo mengi, mnatumalizia karatasi.
 
Back
Top Bottom