Halmashauri ya Ubungo iliwaza nini kumega kipande cha barabara, Mabibo Sokoni na kugeuza Parking?

Halmashauri ya Ubungo iliwaza nini kumega kipande cha barabara, Mabibo Sokoni na kugeuza Parking?

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kwa mara kadhaa nimekuwa nikipita eneo la Mabibo Sokoni, maarufu kama Soko la Ndizi. Kwa muda mwingi, kuanzia unapokata kona kutoka barabara ya Morogoro Road, kumekuwa na msongamano mkubwa wa magari.

1773382127797.png

​
Unaweza kutumia hata nusu saa au saa nzima kupita eneo ambalo kwa kawaida linapaswa kuchukua dakika moja au mbili tu. Leo nilienda sokoni na wife, wakati akiendelea na maemezi nikachukua muda kufuatilia kujua ni nini hasa chanzo cha changamoto hiyo, kwa sababu imekuwa kero kwa miaka ya hivi karibuni.

Nilichogundua ni kwamba Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imechukua sehemu ya barabara na kuifanya maegesho ya magari. Wameweka hata vibao vinavyoonyesha kuwa ni eneo la parking, huku watu wao wanaotoza ushuru wakiwa busy na jukumu hilo.

1773382164095.png
Kuna sehemu unakuta ni maegesho ya bodaboda, maguta, magari ya kawaida, pamoja na maroli. Hali hii imenishangaza na kunifanya nijiulize: mamlaka zimewaza nini? Hawaoni kwamba hili ni tatizo?

Changamoto kubwa inayochangia foleni, licha ya kupunguza upana wa barabara kwa kuifanya kuwa finyu, ni pale dereva wa gari anapotaka kupaki au kutoka katika eneo la maegesho. Wakati huo, magari kutoka pande zote hulazimika kusimama ili kumpisha dereva huyo kukamilisha zoezi hilo.

1773382172603.png
Hali hii imekuwa kero kubwa inayosababisha usumbufu na upotevu wa muda kwa watumiaji wa barabara katika eneo hilo. Napenda kutoa wito kwa mamlaka hususan Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuchukua hatua za haraka kutatua changamoto hiyo ili kupunguza usumbufu kwa wananchi hasa watumiaji vya vyombo vya moto.

Ni vyema watafute eneo lingine la maegesho kama lengo ni kukusanya mapato, badala ya kumega sehemu ya barabara kwa ajili ya matumizi mengine yanayoongeza msongamano (foleni) na usumbufu bila ulazima.

1773382191766.png

1773382204306.png

1773382216318.png

1773382225478.png
 
Bara bara yenyewe Sasa the way ilivyo nyembamba still wameigawa Tena !?

Serikali ya ccm inawaza Kodi tu Pasipo kuja na idea Bora za kutengeneza vyanzo vya ukusanyaji wa Kodi hizo , ,kwani Kwa mfano wange litengeneza Hilo soko la mabibo juu wakaweka rooftop magari yakawa Yana pack huko juu wange pungukiwa Nini !?

Halafu wakati magari hayo yanatoka kwenye rooftop kuingia bara barani wangeweka traffic lights mbona ingekuwa issues simple sana serikali inapenda Hela za watanzania lakini Haina idea mbadala wezeshi za ukusanyaji mapato zinazo endana na uboreshwaji wa Miundombinu
 
Back
Top Bottom