Halmashauri ya urambo yawanyanyasa walimu wapya,haitaki kuwapa mshahara wao na pesa za nauli

MTUNZA AMANI

Senior Member
Joined
Jun 2, 2012
Posts
187
Reaction score
21
Wana jf, ni jambo la kushangaza na kusikitisha kwa hawa maafisa wa wilaya ya URAMBO. Pamoja na walimu kuripoti tarehe mosi aprili,lakini halmashauri haitaki kuwapa mshahara walimu wapya. Imewapendelea walimu wanaojulikana na maofisa na wale wasiojulikana haijawapa mshahara wote badala yake wanapewa laki moja na nusu tu. Ukienda kuuliza hawana majibu ya kueleweka wanajibu wanavojiskia wao. Ikumbukwe hii wilaya ina mazingira magumu,chakula shida n.k walimu hawa wataishije?
 
Ahsante Sam Love, kiukweli inakera sana na inakatisha tamaa ya kufanya kazi. ILA DAWA IPO JIKONI WALIMU AMBAO HAWAJAPATA PESA YAO WAMEPANGA KUANDAMANA HADI KWA MKURUGENZI WA WILAYA ATOE MAJIBU JUU YA SUALA HILI,NA TUTAITA NA WAANDISHI WA HABARI ILI WASAIDIE KUUJULISHA UMA JUU UOZO WA HALMASHAURI YA URAMBO
 
Leo nimeenda halmashauri yana majibu wanayotoa yanaboa sana
 
Kaka mi nipo manispaa hapa tabora, yaliyopo huko ndo yaliyotokea hapa ktambo, tulizungumza na afisa elimu, mayor, hawakuwa na majibu mazuri, tukakutana namkulugenzi nae akapiga kiswahili chakutoa lak na nusu kama mkopo kwan mshahara wetu haujaingia, tukakubaliana kutochukua nakuendelea kugoma huku tukishinikiza kupewa mshahara, usaliti ukatokea miongoni mwetu wenzetu wengi wakatuzunguka wakachukua pesa, ikaonekana tuchukue wote HALAFU KUANZIA JUMATANO NDIO MGOMO RASMI PALE HALMASHAULI ikiambatana na kuwaita waandishi wa habari hadi kieleweke!
 
no right is given on a silver plate....a right must be fought for...pambaneni mpaka kieleweke
 
Yani hawa watu hawafai,hapa ni kupambana mwanzo mwisho.
 
Tunaumia sana. Kaka tupoe wote japo nami nipo Namtumbo ni majanga tu.
 
Watumishi wapya siku zote serikalini huchelewa kuingia kwenye payrall na hivyo kushindwa kupata mshahara wa miez miwili au mitatu ya mwanzo!!

Nyie mmeajiriwa mwez huu tu mnataka mpate salary ilhali hata kwenye payrall hamjaingia na wala check namba hamjapata!! sasa mtalipwaje??

Pia sio kweli kwamba halmashauri haitaki kuwalipa mishahara yenu,kwani nani alokwambia halmashauri ndo inalipa mishahara?? mishahara inalipwa na hazina,na hazina hawawez kukupa mshahara km haupo kwenye payrall na hauna check namba!!!

Hiyo laki moja na nusu ni huruma ya mkurugenz tu kawakopesha ili iwasaidie kwa chakula na mkishaingia kwenye mfumo wa payrall na kuanza kupokea mshahara DED atawakata pesa zake alizowakopesha!!

Kutopata mshahara miez miwili au mitatu ya mwanzo baada ya kuajiriwa serikalini ni jambo la kawaida tu waheshimiwa walimu!!
 

kiongozi umetoa jibu zuri sana tena sana,vijana wasiwe na haraka,binafsi nilikaa miezi 7 ,so vumilien vijana
 
Mimi nimeripoti na nimepewa ila si sababu ya wenzangu kukosa,kifupi ni kuwa kama ulikua hujaripoti tarehe moja hadi tano na kumaliza kujaza mkataba mshahara huu wa kwanza ni ngumu kupata,nasema ivo kwakua nimeambiwa halmashauri na mimi nimepata kwakua nilikamilisha,mshahara wa mwezi wa tano wote lazima mtapata kwaiyo muwe wavumilivu japo inauma sana
 
Uvumilivu? Teh ukimiss mshahara hadi uje udai upewe mvi zimeota
nahilo swala ka tarehe 1 hadi tano si kweli, mi nilireport tarehe 9 nikafungua account NMB tarehe 12 na mwezi huo huo
niapata mshahara, ni ushap tu wa mkurugenzi na watendaji wake...
 

Ulitaka kuandika vizuri ukaboronga unadai mkulugenzi halipi mshahara kwa hiyo mwajili wangu ninani ? nakwanin sijaingia kwenye payral ? huoni
 
Uvumilivu? Teh ukimiss mshahara hadi uje udai upewe mvi zimeota
nahilo swala ka tarehe 1 hadi tano si kweli, mi nilireport tarehe 9 nikafungua account NMB tarehe 12 na mwezi huo huo
niapata mshahara, ni ushap tu wa mkurugenzi na watendaji wake...

Wakurugenzi Wote Walipewa Info Kuwa Walioripoti Na Kumaliza Kujaza Mkataba Siku 5 Za Kwanza Watapata Mshahara Wa Mwezi Wa 4,kinyume Na Hapo Ni Mwezi Ujao
 
Halafu ndugu yangu kwEli we ni lafa eti unatuletea za kukosa mshahara ni kawaida, tatizo eti unadai kawaida thats y tunahitaji kujua tatizo huwa ni nini, pia kujua halmashauri inatusaidiaje kama wafanyakazi wake, by the way kwanin wasitukopeshe mshahara mzima na wakaufuatilia huo wa mwezi wa 4 ndo waukate na wanataka kukata wa mwezi wa tano? jiongeze mkuu usirahisishe hvyo
 
Wakurugenzi Wote Walipewa Info Kuwa Walioripoti Na Kumaliza Kujaza Mkataba Siku 5 Za Kwanza Watapata Mshahara Wa Mwezi Wa 4,kinyume Na Hapo Ni Mwezi Ujao

Walipewa info na nani, lini hiyo....
 
Sijawahi kuona mtu anadai mshahara kabla ya kufanyakazi...
Mnachotakiwa kudai ni subsistence allowance ya siku 7.
 
Ulitaka kuandika vizuri ukaboronga unadai mkulugenzi halipi mshahara kwa hiyo mwajili wangu ninani ? nakwanin sijaingia kwenye payral ? huoni


Mkurugenz ndiyo muajiri , lakini halipi mshahara moja kwa moja,hazina ndiyo wanaolipa mishara ya watumishi wote wa halmashauri na serikali kuu!!

Anachofanya mkurugenzi ni kutuma majina ya watumish wake utumishi na hazina ili waingizwe kwenye payrall chini ya mfumo mpya uitwao LAWSON, mkurugenz hana uwezo wa kuwalipa watumishi ndugu yangu kwan bajet ya mishahara ya watumishi ni kubwa kuliko makusanyanyo ya ndani anayokusanya(own source) ,So sikuboronga ktk maelezo yangu mkuu nipo sahihi kabisa labda nkushauri uende ukailizie kwa DED au DT wa halmashaur yyte atakupa udadavu wa kina kuhusiana na hili!!
 
kiongozi umetoa jibu zuri sana tena sana,vijana wasiwe na haraka,binafsi nilikaa miezi 7 ,so vumilien vijana


Tatizo wakurugenz hawawaelezi vzr hawa waheshimiwa walim wetu jinsi mambo yalivyo!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…