MTUNZA AMANI
Senior Member
- Jun 2, 2012
- 187
- 21
Wana jf, ni jambo la kushangaza na kusikitisha kwa hawa maafisa wa wilaya ya URAMBO. Pamoja na walimu kuripoti tarehe mosi aprili,lakini halmashauri haitaki kuwapa mshahara walimu wapya. Imewapendelea walimu wanaojulikana na maofisa na wale wasiojulikana haijawapa mshahara wote badala yake wanapewa laki moja na nusu tu. Ukienda kuuliza hawana majibu ya kueleweka wanajibu wanavojiskia wao. Ikumbukwe hii wilaya ina mazingira magumu,chakula shida n.k walimu hawa wataishije?