KERO Halmashauri ya Ushetu Idara ya Elimu ya Sekondari wanachelewesha sana fedha za uhamisho

KERO Halmashauri ya Ushetu Idara ya Elimu ya Sekondari wanachelewesha sana fedha za uhamisho

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Watumishi wa Idara ya Elimu ya Sekondari katika Halmashauri ya Ushetu wanaendelea kukumbwa na ucheleweshaji wa malipo ya fedha za uhamisho. Licha ya kupewa ahadi mara kwa mara kuwa malipo yatafanyika, hadi sasa hakuna utekelezaji.

Kinachozua maswali ni kwamba watumishi tuliopangiwa uhamisho pamoja nao kutoka Idara ya Elimu ya Msingi tayari wamelipwa stahiki zao zote, huku sisi wa Sekondari tukiendelea kusubiri bila maelezo ya kuridhisha.

Tunaomba mamlaka husika zitoe ufafanuzi kuhusu sababu za kuchelewa kwa malipo haya na kuhakikisha watumishi wote waliostahili wanalipwa haki zao kwa wakati.
 

Attachments

Changamoto ya malipo ya stahiki za uhamisho katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, hasa kwa watumishi wa Idara ya Sekondari, ni kubwa. Watumishi wanahamishwa bila kulipwa stahiki zao, na wanapofuatilia malipo hayo huonekana kama kero. Wakati huo huo, watumishi wa Idara ya Msingi hulipwa stahiki zao kwa wakati.

Kiuhalisia, Idara ya Sekondari inawatendea watumishi isivyo haki, ilhali nao wana familia na majukumu kama viongozi wa idara wanavyokuwa nayo.
 
Back
Top Bottom