Changamoto ya malipo ya stahiki za uhamisho katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, hasa kwa watumishi wa Idara ya Sekondari, ni kubwa. Watumishi wanahamishwa bila kulipwa stahiki zao, na wanapofuatilia malipo hayo huonekana kama kero. Wakati huo huo, watumishi wa Idara ya Msingi hulipwa stahiki zao kwa wakati.
Kiuhalisia, Idara ya Sekondari inawatendea watumishi isivyo haki, ilhali nao wana familia na majukumu kama viongozi wa idara wanavyokuwa nayo.