Davidmmarista
JF-Expert Member
- Apr 11, 2024
- 3,114
- 6,309
TAARIFA KWA UMMA
KUKANUSHA TAARIFA YA KUDHALILISHWA KWA MWALIMU OMARI SALIMU ALLI
Mwalimu Omari Salimu Alli ni mtumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Siha aliyeajiriwa tarehe 01/04/2014. Baada ya ajira alipangiwa kituo cha kazi shule ya Sekondari Karansi ambapo amefanya kazi kwa muda wa miaka kumi na moja (11). Mnamo tarehe 07/11/2025 alihamishwa kituo cha kazi kwa barua yenye Kumb. Na. SDC/PF.1437/26 kutoka Shule ya Sekondari Karansi kwenda Shule ya Sekondari Dahani (Uhamisho wa kawaida wenye lengo la kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma ya ufundishaji).
Mwalimu Omari aliomba kulipwa gharama za uhamisho na Mwajiri alitambua stahiki yake yenye thamani ya shilingi 5,688,000.00 na kumjulisha kwa barua yenye Kumb. SDC/PF.1437/39 ya tarehe 10/03/2026 kuwa angelipwa kadri fedha zinavyopatikana. Hata hivyo mwalimu Omari alikaidi kuanza kazi katika kituo kipya kwa maelezo kuwa hawezi kufanya hivyo hadi atakapolipwa gharama zote za uhamisho. Halmashauri imelipa madai na madeni ya gharama za uhamisho zenye thamani ya shilingi 198,345,700.00 kwa awamu nne kwa walimu wa sekondari thelathini na mbili (32). Aidha Mwalimu Omari alilipwa stahiki za Uhamisho zenye jumla ya shilingi 5,688,000.00 kwa awamu nne kama ifuatavyo:
Katika kipindi chote cha malipo ya awamu tatu za mwanzo Mwajiri amekuwa akimtaka Mwl. Omari kwenda kituo chake kipya cha kazi kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma lakini aliendelea kukaidi maelekezo halali ya Mwajiri pamoja na kuendelea kupokea mshahara ambao amekuwa haufanyii kazi. Kwa busara ya Mwajiri aliacha kumchukulia hatua za kinidhamu hadi atakapokamilisha malipo yake. Baada ya Mwajiri kukamilisha stahiki za uhamisho za mwalimu Omari alimtaka kwenda kwenye kituo chake kipya ili kuendelea na kazi.
Hatua hii ni pamoja na kukabidhi nyumba ya shule ya Sekondari Karansi kwa Mkuu wa Shule ili kupisha nyumba hiyo itumike na mtumishi mwingine wa kituo hicho (Maelekezo haya yalitolewa kwa barua yenye Kumb. Na. SDC/WPF.1437/17 ya tarehe 18/08/2026 iliyompa siku 14 za kukabidhi nyumba ya shule ya Sekondari Karansi).
Pia mwalimu Omari aliwasilisha ombi la kuhamia Halmashauri ya Jiji la Tanga ambapo alipewa maelekezo ya kufanya maombi ya uhamisho kupitia Mfumo wa ESS kwa barua yenye Kumb. Na. SDC/WPF. 1437/02 ya tarehe 08/06/2026. Mwajiri aliwaelekeza wataalam wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu kwa kushirikiana na wataalam wa TEHAMA kumpa ushirikiano ili akamilishe ombi la uhamisho. Mwalimu Omari alifika ofisini na kusaidiwa kuomba uhamisho kwenye mfumo wa ESS na mfumo ulionesha hakukuwa na nafasi ya cheo chake katika Halmashauri ya Jiji la Tanga. Kutokana na changamoto hiyo Wataalam wa Utumishi na TEHAMA walimshauri Mwalimu Omari kuomba Halmashauri nyingine zilizopo Mkoa wa Tanga lakini alikataa na kusisitiza kuwa ni lazima aende Jiji la Tanga.
Mwalimu Omari aliendelea kukaidi maagizo ya mwajiri hali iliyopelekea hatua ya kumtoa kwenye nyumba ya shule ya Sekondari Karansi mnamo tarehe 12/09/2026. Aidha, hadi kufikia 21/09/2026 mwalimu Omari hayupo kwenye kituo kipya cha kazi(Sekondari ya Dahani), hivyo Mwajiri kwa kushirikiana na Mamlaka ya nidhamu kwa Walimu wanaendelea kulifanyia kazi suala hili kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma.
Halmashauri ya Wilaya ya Siha inatoa wito kwa Watumishi, Wananchi na Wadau mbalimbali kutopotoshwa na taarifa zisizo za kweli. Pia Halmashauri inawahakikishia kuwa itaendelea kusimamia Haki na Maslahi ya Watumishi wa Umma pamoja na kuendelea kutoa huduma kwa wananchi kwa weledi na Ufanisi.
Imetolewa na:
Macha
Modesta C. Kitunguye
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
21/09/2026
Soma pia Kilimanjaro: Mwalimu agomea kuhama, vitu vyake vyatolewa nje Siha