Halmashauri ya Wilaya ya Ileje lipeni pesa za kujikimu

Halmashauri ya Wilaya ya Ileje lipeni pesa za kujikimu

Supu ya kokoto

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
4,194
Reaction score
7,602
Ndugu wanabodi.

Hali ni tete kwa sisi ajira mpya kada ya elimu na afya kwenye halmashauri ya wilaya ya Ileje. Fedha za kujikimu zimeshatolewa, waraka umetoka, wamekaa vikao kuzigawa katika vifungu kwa mujibu wa taratibu zao. Pesa ziko tayari yapata wiki mbili nyuma.

Tunaombeni mtulipe huku vijijini tunakufwaa hatuna mahitaji. Tuoneeni huruma.
 
Ileje huwa Kuna ukiritimba Sana hasa hospitali ya itumba DMO na katibu wake Kuna shida mahali. Ukijifanya kusema Sana wanakupanga vijijini kabisa.

Nimefanya kazi itumba muda flani kabla sijahama Kuna upuuzi mwingi Sana.
 
Ndio wapi uko
Mkoani Songwe. Mkuu tusaidieni kupaza sauti tulipwe pesa za kujikimu,imagine tuko ugenini,vijijini na tunakoenda kufuata mahitaji (itumba,isongole) kwa pikipiki ni almost 30,000/ kwenda tuu.
 
Mkoani Songwe. Mkuu tusaidieni kupaza sauti tulipwe pesa za kujikimu,imagine tuko ugenini,vijijini na tunakoenda kufuata mahitaji (itumba,isongole) kwa pikipiki ni almost 30,000/ kwenda tuu.
Poleni natumai DMO ndugu Joyce ongati atawasaidia kupata stahiki zenu maana wandali wakikujua wewe ni mgeni vitu wanapandisha Bei.
 
Leo bado holaaa....tunaambiwa mfumo wa BOT umegoma kuruhusu malipo. Twafaaaaa
 
Back
Top Bottom