The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida imekabidhi mikopo ya Sh. milioni 395 kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,Asia Messos,akizungumza jana wakati wa hafla ya kutoa mikopo hiyo alisema baada ya dirisha kufunguliwa jumla ya vikundi 143 vilituma maombi ambapo vikundi 73 vimefanikiwa kupata mikopo hiyo katika awamu ya kwanza ambapo katika vikundi hivyo vilivyopata mkopo vya wanawake 51, vijana 19 na vikundi 3 vya watu wenye ulemavu.
Soma Pia: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Naye Mbunge wa Iramba Mashariki, Francis Mtinga, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo alitoa wito kwa vijana, wanawake na watu wenye ulevamavu wilayani Mkalama kutumia vizuri mikopo wanayopewa kwa kuwekeza katika biashara zenye tija ili waweze kujikwamua kiuchumi na kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.

Picha: Nipashe