KERO Halmashauri za Wilaya za Kilimanjaro hazijatulipa posho ya kujikimu sisi Ajira mpya

KERO Halmashauri za Wilaya za Kilimanjaro hazijatulipa posho ya kujikimu sisi Ajira mpya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nimeogopa kutaja directly kituo cha kazi huwenda nikajulikana

Lakini,

Muda mrefu umepita Baada ya kuripoti ila ni kama wanapotezea posho ya kujikimu wakati ipo kwa mujibu wa Sheria.

Tumewasiliana na wenzetu wa Halmashauri zingine tukagundua hili ni tatizo la Halmashauri zote za mkoa wa Kilimanjaro.

Tunaomba Msaada, Serikali ngazi za juu iingilie kati tafadhali.
 
Wanakuambia, "Nyinyi mlikuwa mtaani mnateseka na maisha, hamna hata hela ya kula, leo hii serikali imewaonea huruma imewaajiri, mnaanza kuona eti inawatesa kwa kutowapa hiyo hela ya kujikimu"
 
Andika barua, "tafadhali taja mkurugenzi" kuwa nakumbushia malipo ya hela ya kujikimu,
 
Hivi posho ya kujikimu kwa afisa maendeleo ya jamii huwa ni Shngapi?
 
Hicho ni kilio kila halmashauri, ila baadhi ya halmashauri zenye mapato makubwa kama za jiji zimewalipa ajira mpya
 
Halafu mbona kelele za halmashauri ni nyingi Sana, sidhani hata milioni inafika ya mshahara halafu bado mnazungushwaa, Kwa Hali hiyo huko makazini kwenu mtafanya kazi kweli Kwa Hali hiyo?, huwezi kufanya kazi vizuri kwa staili hiyo.
 
Nimeogopa kutaja directly kituo cha kazi huwenda nikajulikana

Lakini,

Muda mrefu umepita Baada ya kuripoti ila ni kama wanapotezea posho ya kujikimu wakati ipo kwa mujibu wa Sheria.

Tumewasiliana na wenzetu wa Halmashauri zingine tukagundua hili ni tatizo la Halmashauri zote za mkoa wa Kilimanjaro.

Tunaomba Msaada, Serikali ngazi za juu iingilie kati tafadhali.
Tafadhali kuweni na subira kidogo, serikali itawalipa tutakapouza dhahabu yote kule bot..
 
Back
Top Bottom