Halmashauri ziruhusiwe zilipe watumishi wake kadri ya makusanyo kama ilivyo kwa mashirika ya umma

Davan

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2020
Posts
1,125
Reaction score
1,413
Ukiuliza kwanini mashirika ya umma mishahara yao ni tofauti na wizara na halmashauri utaambiwa haya mashirika yanazalisha fedha kwa serikali na kujiendesha.

Tuje kwa halmashauri huku kuna tofauti kubwa ya makusanyo kati ya halmashauri moja na nyingine lakini mishahara ya watumishi wote wa halmashauri ni sawa kwa kada husika nchi nzima.

Hebu angalia makusanyo ghafi mwaka 2018/2019
ILALA 58B
K/NDONI 34B
TEMEKE 33.3B
NANYAMBA 257.6MILL

Pamoja na makusanyo hayo bado afisa biashara wa ilala yuko scale moja na afisa biashara wa Nanyamba.

Kwanini mashirika yajipangie mishahara lakini halmashauri haziruhusiwi?
Kama nchi kuna sehemu tumekosea. Hili swala linahitaji mjadala wa kina.
 
Haya mambo ya watu kujipangia mishahara inabidi sisi wananchi ambao ndio mabosi wao tuwapangie...., eti makusanyo !!!!, bora kama ni kweli yanazalisha na kweli yanajiendesha (yaani kodi yetu haitumiki) ila kukusanya nako kunahitaji jitihada mi naona yule inyokusanywa kutoka kwake ndio ajipangie awape wakusanyaji ngapi....
 
Tunarudi kulekulee kwa Lissu na mambo ya decentralization na uongozi wa majimbo.

Hivi ndivyo ilivyotakiwa kuwa lkn kuna tatizo 1, raia wako mbele kifikra kuliko serikali. Yani ni sawa na kusema raia tunatumia iphone 12 pro max lkn serikali bado iko kwenye iphkne 6s.
 
Halmashauri zikishindwa kuwalipa mishahara watumishi wanawapa redunduce
 
Haya mambo ya watu kujipangia mishahara inabidi sisi wananchi ambao ndio mabosi wao tuwapangie...., eti makusanyo !!!!, bora kama ni kweli yanazalisha na kweli yanajiendesha (yaani kodi yetu haitumiki) ila kukusanya nako kunahitaji jitihada mi naona yule inyokusanywa kutoka kwake ndio ajipangie awape wakusanyaji ngapi....
Janja janja hii ilianza awamu ya late Mkapa ikawa fungulia mbwa kila shirika na mshahara wake
 
Kwa hiyo karani wa kukusanya ushuru apewe kiasi gani maana naye ni mtu muhimu sana katika makusanyo
 
Mshahara uwe sawa labda kua na bonus kutokana na kufikia target iliyopangwa na halmashauri kutokana na resources zake. Mapato ya Nanyamba hayawezi kufikia Ilala hata hao watumishi wawapore hao wakazi pesa zao zote hawawezi pata kiasi sawa na Ilala.
 
Maana yake mnashauri halmashauri zilipe zenyewe watumishi wake mishahara?

........Au mimi ndio nipo nyuma na uelewa?
 
Hoja yangu hapa taasisi zinazoingiza pato kubwa kwa serikali mishahara yao ni mikubwa ukilinganisha na halmashauri ila halmashauri zinazoingiza mapato makubwa bado watumishi wake wanalipwa sawa na halmashauri zinazoingiza kidogo. Kwanini?
 
Ukiuliza kwanini mashirika ya umma mishahara yao ni tofauti na wizara na halmashauri utaambiwa haya mashirika yanazalisha fedha kwa serikali na kujiendesha.

Tuje kwa halmashauri huku kuna tofauti kubwa ya makusanyo kati ya halmashauri moja na nyingine lakini mishahara ya watumishi wote wa halmashauri ni sawa kwa kada husika nchi nzima.

Hebu angalia makusanyo ghafi mwaka 2018/2019
ILALA 58B
K/NDONI 34B
TEMEKE 33.3B
NANYAMBA 257.6MILL

Pamoja na makusanyo hayo bado afisa biashara wa ilala yuko scale moja na afisa biashara wa Nanyamba.

Kwanini mashirika yajipangie mishahara lakini halmashauri haziruhusiwi?
Kama nchi kuna sehemu tumekosea. Hili swala linahitaji mjadala wa kina.
tulia halmashauri huko huko ukitaka na wewe hamia TPA au nasema uongo ndugu zanguuu
 
Hebu jaribu kuvuta picha, halmashauri ya Bumbuli makusanyo ya Mwaka 2019 ni 186 Million. je, yanatosha kuwalipa watumishi wake mishahara pamoja na matumizi mengineyo?
Hapo utakuwa mwanzo wa watumishi wengi kukimbilia halmashauri zinazolipa vizuri zaidi.
 
Nini kifanyike kwa haya mashirika yanayojilipa vizuri sababu wao wanaingiza mapato serikalini?
 
Acha iwe hivi hivi tu...
Sababu pakiwa na mataba patakua na ukiritimba sana...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom