UTANGULIZI
Halmashauri nyingi nchini zimekua zikitumia vyanzo vya mapato vile vile miaka yote, hakuna ubunifu wa vyanzo vipya, halmashauri nyingine zimekua mizigo kwa Serikali kwa kutegemea fedha nyingi kutoka Serikali kuu ili kujiendesha huku zikiwa na vyanzo vingi vya mapato ambavyo havitumiki. Nashauri MAENEO yafuatayo yaguswe kupata mapato zaidi ya Serikali :
1. Biashara ya Nyumba za kupanga za makazi irasimishwe
Nashauri biashara ya nyumba za kupanga nchini kote irasimishwe na wapangishaji wote wawe na leseni pia serikali itoze angalau asilimia 20% ya kodi pia wapangaji wawe wanalipia kodi kwa utaratibu rasmi wapewe na risiti na MIKATABA yao ikaguliwe
(Anuani za makazi tayari zitakua zimesaidia kurahisisha zoezi hili kwa kutambua nyumba zinazofanya biashara ya kupangisha, ANGALIZO: kodi hii iwe ni maalumu kwa nyumba zinazopangishwa kwa ajili ya makazi na biashara tu).
Humu kwenye nyumba za kupanga za makazi Serikali inapoteza mabilion ya pesa kila mwezi mfano mimi ninapoishi nmepanga nalipia Tshs. 150,000/= kila mwezi(vyumba viwili na sebule) ila serikali haipati hata mia mbovu kwenye pesa hiyo. Wapo watu wanalipia kodi mpaka 1,000,000 kwa mwezi mmoja ila Serikali haipati kitu. Hii ni biashara lazima Serikali ikusanye na ifanyike kwenye nyumba za kibiashara pia maarufu kama fremu.
Kodi hizi za nyumba za kibiashara na za kupangisha baada ya wapangishaji kukaguliwa mikataba yao, watendaji wa kata watumike kukusanya mapato hayo ya halmashauri kwa njia za kielekroniki(wapewe mashine za EFD) na pia iwapo mpangaji akiwa anataka kuhama au anahama mpangishaji atoe taarifa hiyo kabla ya mwisho wa mwezi (kwa. Mujibu wa mkataba wa mpangaji) unaofuata toka kuhama mpangaji na afisa wa halmashauri ngazi ya kata athibitishe na kuripoti nakala kwa mwajiri wake(halmashauri).
Pia iwe ni kosa kisheria kupangisha nyumba kwa ajili ya makazi au biashara bila kuwa na leseni, faini isipungue shilingi za kitanzania milioni moja.
2. Halmashauri ziwekeze kwenye miradi ya kimkakati ya biashara maeneo yenye uhitaji.
Serikali bado inakosa fedha nyingi kwa kukosa maono, kuna maeneo mengi mfano Kuna uhaba wa Kumbi za sherehe, magari ya abiria, vituo vya mafuta, wakala wa kifedha, nyumba za kulala wageni nk Serikali inaweza kujenga au kuwekeza huko na kupata mapato makubwa mno. Mfano uhitaji wa nyumba za kulala wageni kwenye miji ya kimkakati kama Dodoma mjini, Dar, Arusha na jirani na stendi karibu zote za kimkakati hakuna za gesti za Serikali kwanini?
3. Kuta za uzio za mashule, vyuo na baadhi ya maofisi yaliyo katikati ya miji zitumike kibiasharara.
Mfano shule ya sekondari Uhuru (ya Serikali) iliyopo Shinyanga mjini imezungushiwa ukuta wenye eneo zuri mno la kujenga vyumba vya biashara zaidi ya 200 lakini hautumiki cha kusikitisha kwenye shule hiyo hata chaki zikiisha Serikali inanunua.
4. Halmashauri zikodishe mitambo na vifaa vya kitaalamu kuongeza mapato.
Kwenye halmashauri nyingi nchini ujenzi unaendelea wa miradi mingi na majumba binafsi lakini halmashauri hazinufaiki moja kwa moja na ukuaji wa shughuli hizo kwa kushiriki kiufundi kuchochea upatikanaji wa vitendea kazi kwa kuvikodisha na kupata mapato mengi. Hili ni tatizo karibu halmashauri zote nchini
5. Maeneo ya wazi ya Serikali yaliyotengwa kwa matumizi fulani ya baadae kama matumizi halisi mda wa utekelezaji bado sana yawekewe mipango ya matumizi ya dharura kuchochea shughuli za kiuchumi na kuongeza mapato kwa Serikali. Mfano maeneo mengi ya hifadhi ya reli na barabara ambayo hayatarajiwi kuendelezwa leo wala kesho yaliyo maeneo ya mijini yatumike kukodishia wajasiriamali wadowadogo kwa biashara ndogo ndogo kodi zikusanywe.
6. Serikali iwe ya kwanza kuvuna rasilimali za nchi.
Hapa ni kwenye rasilimali za kimkakati kama madini, halmashauri zetu ziunde kampuni mfano za uchimbaji (ndogo au kubwa) kwa kutumia wataalamu wa ndani walioajiriwa na halmashauri hizo ili halmashauri ziwe za kwanza kuchangamkia fursa mbalimbali ambapo itasaidia kuzalishia halmashauri husika mapato makubwa mno. Kwa mfano kwenye sekta ya madini kwa sasa halmashauri zetu zinachoambulia ni fedha ya fadhila kwa jamii (CSR) pekee huku makampuni ya uchimbaji ambayo mengi ni kutoka nje yakivuna utajiri mkubwa kwenye halmashauri hizo kwa mfano halmashauri ya Kishapu ulipo mgodi wa Mwadui na El Hilal kunakochimbwa almasi halmashauri hiyo ni moja kati ya halmashauri zenye uchumi dhaifu zaidi nchini wakati ina utajiri mkubwa wa madini.

Upvote
3