A
Anonymous
Guest
Naishi Zanzibar, Mkoa wa Mjini Magharibi, Wilaya ya Magharibi B, ni mtumiaji wa Mtandao wa Halotel kwa takribani miaka nane sasa, lakini kwa kipindi hiki nimekuwa nikikumbana na changamoto ya kutopatikana kwa huduma ya mtandao katika baadhi ya maeneo.
Nikifanya safari kutoka Mkoa wa Mjini Magharibi kuelekea Mkoa wa Kaskazini, mara nyingi mtandao hausomi kabisa. Nimewahi kuwasiliana na huduma kwa wateja na kuambiwa huenda tatizo likawa kwenye simu yangu. Nilinunua simu mpya, lakini bado changamoto hiyo imeendelea kuwepo.
Hata leo, nimetoka ninapoishi na kusafiri takribani kilomita 20, lakini huduma ya mtandao bado haipatikani katika baadhi ya maeneo. Hali hii inatukwaza sana sisi watumiaji ambao tunategemea huduma hiyo kwa mawasiliano na shughuli mbalimbali za kila siku.
Tunaomba Halotel iboreshe huduma zake na kuhakikisha mtandao unapatikana kwa uhakika katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar na nchi nzima. Tumekuwa wateja kwa muda mrefu, lakini changamoto ya kutopatikana kwa huduma inatufanya tukose imani na huduma mnazotupatia.