Halotel: Itatoboa kwa vodacom, airtel, tigo,ttcl?

AAS

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2015
Posts
330
Reaction score
35
Habari ya mapumziko wana jukwaa!!!

Hivi karibuni imezinduliwa kampuni mpya ya mawasiliano inayokwenda kwa jina la Halotel. Inakuja kumenyana kibiashara na kampuni kubwa na ambazo zimejiimarisha kwa muda mrefu hapa nyumbani na nje ya nchi yakiwemo tigo,ttcl, airtel,vodacom na mengineyo.

Hebu tujiulize ni nini wamekiona mpaka wakaamua kuingia katika soko hili ambalo tayari lina ushindani mkubwa kiasi hiki?
Hii ni kampuni ambayo inamilikiwa na jeshi la Vietnum, je ndio maana si waoga kwenye kuwekeza sababu hizi fedha ni za umma? na je ni kwa sababu hata zikipotea hamna mtu ataweza kupata maumivu ya hasara hiyo moja kwa moja? je wateja wao ni kina nani sababu kila mwenye simu tayari ana line ya hizo kampuni kubwa na hata anayenunua simu leo ni vigumu kuanza na line ya mtandao ambao ndio kwanza unajenga minara.

Halotel wamekuja kuwekeza kiasi cha takribani dola 736 million za Marekani (sawa na tsh 1.62 trilion). je pesa hizi zingekua zako ungeweza kuiona fursa hii na kuziwekeza hapa Tanzania? Ukiweka maanani kwamba kuna kampuni zipo tayari kwa miaka mingi hapa nchini zikitoa huduma ya mawasiliano lakini bado hazijaweza kushika soko ipasavyo.

Kama si kwenye biashara ya kampuni ya mawasiliano, je ungethubutu kuziwekeza kwenye biashara/sekta gani hapa nchini?

Karibuni tujadili.




 
Naona idara ya masoko imeshindwa kufanya kazi kabisa. Hawakuniandaa kuanza. Hawakutakiwa kianza kimya na kichovu namna hiyo. Wamwite Mafuru awazindue.
 
Naona idara ya masoko imeshindwa kufanya kazi kabisa. Hawakuniandaa kuanza. Hawakutakiwa kianza kimya na kichovu namna hiyo. Wamwite Mafuru awazindue.
kwa hiyo idara ya masoko ikisimama wanaweza shindana na hizi kampuni kongwe?
 
Hawana ofa za kumshawishi mtu aachane na voda/tigo/airtel, tigo kipindi kile inaanza ikijuwa na ofa nzur kwa wateja wake kama vile kupiga simu bure muda wa usiku, kuongea kwa nusu shiling kwa dakika nk.
Halotel wajitahidi kwa kuweka ofa nzuri zitakazowashawishi watu kuachana na mitandao iliyokuwepo sasa, wajitangaze sana kwenye tv stations na media nyinginezo. Page yao facebook imepooza sana.
 
hawa jamaa walichopatia ni kitu kimoja tu,
wameanzia vijijini.wameweka minara yao sehem ambazo hupati tigo,vda,wala airtel.pia hata ukiwa kijijin kiasi gani unapata 3G,hivyo watu wanashawishika kwa hili tofauti na mtandao wa smart upo dar tu na mikoa mikubwa mikubwa.
wakijipanga kwenye matangazo na wakaongeza ofa kubwa hata kwa miaka miwili watazoa wateja
 
Wamekuja wakati mbaya sana.

Oligopoly ya Vodacom, Tigo na Airtel wameikamata TCRA vilivyo.

Hawawezi kupindua kwa kutoa offer za kuvutia wateja.
 

ok sawa mkuu nimekupata ila kushusu kujitangaza naona wanpaka rangi yao kwenye nyumba nyingi sana hasa ukitoka dar to arusha wamejitahidi sana

vipi wakijaribu kijikita kwenye huduma za internet zaidi sababu hawa waliopo wameonesha kubana vifurushi sana hawatawashika hapo
 
Wamekuja wakati mbaya sana.

Oligopoly ya Vodacom, Tigo na Airtel wameikamata TCRA vilivyo.

Hawawezi kupindua kwa kutoa offer za kuvutia wateja.

ok mkuu sawa hpo kwenye oligopoly umeniacha hii ni nini?

inachangia vipi wao kutocompete na hawa waliopo?

ni mbinu ya kisayansi au ni fitina za biashara?

sababu wabongo wanaweza kukukwamisha kwa fitina hata km una strategy kubwa kiasi gani
 

ok na nafikiri moja kati ya vigezo vilivyowafanya wapate kibali ni kupeleka mawasiliano vijijini

lakini hii nayo vipi sababu naona kukua kutoka kijiini kidogo ni ngumu kuliko kukua kutoka mjini si kwamba hii itawachelewesha? mfano ktk miji mikubwa ndipo mahali kwenye watu wengi watumiaji wakubwa wa huduma za simu na internet. hata kampuni nyingi utakuta makao makuu ni dar mikoani ni branch tu
 
Kwa mishahara mbuzi yao kwa Engineers na wengine hawatafika mbali
 
Hakuna kitu hapo. Nilipoona tu kampuni yenyewe imeanza kwa kujiingiza kwenye biashara ya kuuza MB 3 nikaona tayari hawa ni walewale kasoro majina.
 
Hii kampuni inaubia na mstaafu na Ina mkataba wa kufunga net kwenye halmashauri zote nchini baada ya Muda mfupi tu pesa Yao itakuwa imerudi.
 
Wamekuja wakati mbaya sana.

Oligopoly ya Vodacom, Tigo na Airtel wameikamata TCRA vilivyo.

Hawawezi kupindua kwa kutoa offer za kuvutia wateja.
Mkuu nikweli,mimi nimezungumza nao inaonekana wamewekewa gavana/spana na TCRA - walinishangaza waliposema hawawezi kwenda kinyume na charges za makampuni ya simu nchini!

Hii inamaanisha kampuni hizi za simu Nchini zinaendesha biashara zao kwa mtindo wa ki-cartel hivi ambao ni kinyume cha sheria!

Tunambiwa Tanzania inaruhusu Biashara huria lakini naona kitu hicho hakipo kwenye Makampuni ya simu yanaonekana kuiteka nyara TCRA, shinikizo la makampuni ya simu nchini ndio kumeifanya HALOTEL ifuate mkumbo bila hilo tarrifs zao zingekuwa chini/nafuu mno.

Naona Dk.Magufuli atapaswa kutupia macho makampuni haya ya Simu vile vile na utendaji kazi wa TCRA una walakini sana hawaweki maanani maslahi ya wateja/watumiaji6 wa simu.
 
Biashara kubwa ya mitandao ya simu siku hizi ni bando,

Bando zao zina gharama sana kufanya watu wasiwaunge mkono though internet yao ipo vizuri
 
Watu wengi tunataka bundle, sasa hawana tofauti na hao wakongwe. Yaani wao wanaanza afu wanaweka mb 3
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…