babu M
JF-Expert Member
- Mar 4, 2010
- 5,222
- 3,173
This is ridiculous......Hizo dola 736 million za Marekani wanawekeza kwenye nini? Wakati mikonga yenyewe niya kukodisha!Habari ya mapumziko wana jukwaa!!!
Hivi karibuni imezinduliwa kampuni mpya ya mawasiliano inayokwenda kwa jina la Halotel. Inakuja kumenyana kibiashara na kampuni kubwa na ambazo zimejiimarisha kwa muda mrefu hapa nyumbani na nje ya nchi yakiwemo tigo,ttcl, airtel,vodacom na mengineyo.
Hebu tujiulize ni nini wamekiona mpaka wakaamua kuingia katika soko hili ambalo tayari lina ushindani mkubwa kiasi hiki?
Hii ni kampuni ambayo inamilikiwa na jeshi la Vietnum, je ndio maana si waoga kwenye kuwekeza sababu hizi fedha ni za umma? na je ni kwa sababu hata zikipotea hamna mtu ataweza kupata maumivu ya hasara hiyo moja kwa moja? je wateja wao ni kina nani sababu kila mwenye simu tayari ana line ya hizo kampuni kubwa na hata anayenunua simu leo ni vigumu kuanza na line ya mtandao ambao ndio kwanza unajenga minara.
Halotel wamekuja kuwekeza kiasi cha takribani dola 736 million za Marekani (sawa na tsh bilioni 16.9). je pesa hizi zingekua zako ungeweza kuiona fursa hii na kuziwekeza hapa Tanzania? Ukiweka maanani kwamba kuna kampuni zipo tayari kwa miaka mingi hapa nchini zikitoa huduma ya mawasiliano lakini bado hazijaweza kushika soko ipasavyo.
Kama si kwenye biashara ya kampuni ya mawasiliano, je ungethubutu kuziwekeza kwenye biashara/sekta gani hapa nchini?
Karibuni tujadili.
Hawa wanakuja na figure kubwa ili watukamue kwenye kodi.