HOJA Halotel itoe ufafanuzi kuhusu kuchelewa kwa malipo ya kamisheni ya Mawakala wa HaloPesa

HOJA Halotel itoe ufafanuzi kuhusu kuchelewa kwa malipo ya kamisheni ya Mawakala wa HaloPesa

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Mawakala wakuu wa mtandao wa Halotel Tanzania upande wa HaloPesa, tunaiomba kampuni itolee ufafanuzi kuhusu kucheleweshwa kwa malipo yetu ya kamisheni bila sababu za msingi.

Awali tuliambiwa kuwa malipo yangefanyika baada ya kuwasilisha risiti za EFD kutoka TRA. Tumezifikisha risiti hizo tangu tarehe 3, lakini hadi leo hatujapokea malipo wala taarifa yoyote kuhusu hatua iliyofikiwa.

Hali hii inatuletea changamoto kubwa kwa kuwa tunapaswa kulipa mishahara ya wafanyakazi wetu pamoja na kutekeleza majukumu ya kodi kwa TRA. Tunaomba kampuni ishughulikie suala hili haraka na kutupatia mrejesho kuhusu malipo yetu.
 
Back
Top Bottom