Halotel mjitafakari mmebakia nyie

Halotel mjitafakari mmebakia nyie

NITAKUKAMATA TU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2021
Posts
347
Reaction score
432
Habari ndugu wanajamvi.

nitoe pole pole za dhati kwa watanzania WOTE ,kutokana na msiba na janga La kuanguka kwa jengo La kariakoo.
Baada ya pole hiyo, nipende kutoa malalamiko YANGU kwenda kwa mtandao WA laini za simu, kampuni ya HALOTEL.

Kampuni hii imeshindwa kulinda wateja wake kwa kuruhusu ,watu tusio watambua kututumia meseji za UGANGA,KUJIUNGA FREEMASON,TUMA NAMBA HII,KUUNGANISHWA NA HUDUMA biła ridhaa yetu,mfano-HALOSOKA,na sms zingine zinazoendana na hizo.

Jambo hili La kupokea jumbe za namna hiyo kupitia laini ya halotel,limekuwa mara kwa mara likijitokeza na kuwa kero kwa baadhi yetu.

HII ni tofauti na mitandao mingine ambayo meseji za namna hiyo ni agharabu kuziona.

Natoa Lai kwa mtandao WA halotel ,kupambana kututatulia jambo Ili na kuzuia namba zetu kuweza kujulikana na watu hao wanaotutumia jumbe biła lidhaa yetu.

Asanteni
 
Hebu jifunze kwanza kuandika:
1. Tambua matumizi sahihi ya herufi kubwa na usichanganye na herufi ndogo kwenye sentensi.
2. Lai = Rai
3. Jambo ili = Jambo hili
4. Lidhaa = Ridhaa.
Pamoja na changamoto hiyo hapo juu lakini ulichosema ni sahihi.
Hao jamaa hawana adabu. Hata mimi Nabii wananitumia jumbe za kiganga. Leo wamenitumia ujumbe huu:
"Shemeji hii ndio namba ya yule mganga alienisaidia ana uwezo mkubwa sana wa kutoa mali bila kafara, kurudisha mke au mume PETE ya bahati na kutibu magonjwa yote. mpigie 0680261815"
 
Unazan kuna mashindano ya kuandika hapa jf, au unajua wakati MTu anaandika unakuta Yuko Katika mood gan? Mkiisha ona ka dosari ndio inakuwa point kujitia big brain
 
Pamoja na changamoto hiyo hapo juu lakini ulichosema ni sahihi.
Hao jamaa hawana adabu. Hata mimi Nabii wananitumia jumbe za kiganga. Leo wamenitumia ujumbe huu:
"Shemeji hii ndio namba ya yule mganga alienisaidia ana uwezo mkubwa sana wa kutoa mali bila kafara, kurudisha mke au mume PETE ya bahati na kutibu magonjwa yote. mpigie 0680261815"
Kiukweli mwanajamii wajiekebishe
 
Habari ndugu wanajamvi.

nitoe pole pole za dhati kwa watanzania WOTE ,kutokana na msiba na janga La kuanguka kwa jengo La kariakoo.
Baada ya pole hiyo ,nipende kutoa malalamiko YANGU kwenda kwa mtandao WA laini za simu, kampuni ya HALOTEL.

Kampuni hii imeshindwa kulinda wateja wake kwa kuruhusu ,watu tusio watambua kututumia meseji za UGANGA,KUJIUNGA FREEMASON,TUMA NAMBA HII,KUUNGANISHWA NA HUDUMA biła ridhaa yetu,mfano-HALOSOKA,na sms zingine zinazoendana na hizo.
Jambo hili La kupokea jumbe za namna hiyo kupitia laini ya halotel,limekuwa mara kwa mara likijitokeza na kuwa kero kwa baadhi yetu.

HII ni tofauti na mitandao mingine ambayo meseji za namna hiyo ni agharabu kuziona ,

Natoa Lai kwa mtandao WA halotel ,kupambana kututatulia jambo Ili na kuzuia namba zetu kuweza kujulikana na watu hao wanaotutumia jumbe biła lidhaa yetu.
Asanteni
Mkuu,

Unajuaje tatizo lipo Halotel?

Tanzania watu wanatoa namba sana, kila sehemu ukienda unaandika namba ya simu.

Vipi kama kuna watu wanazikusanya hizi namba na kuzitumia kwa mass marketing bila ya kupata namba kutoka Halotel?

Naelewa Halotel wanaweza kuweka anti spamming measures, lakini zaidi ya hapo kama watu wanatoa namba kirahisi yu, ukienda ofisi yoyote unawaachia namba yako, unajuaje kama hawauzi hizo namba?
 
Mbona mie kwa upande wangu nazipata sana kutoa namba za TTCL. Ila nawapiga spana sana kila jumbe ya kitapeli nairipoti kwenye ile namba 15040 ya TCRA
 
Pamoja na changamoto hiyo hapo juu lakini ulichosema ni sahihi.
Hao jamaa hawana adabu. Hata mimi Nabii wananitumia jumbe za kiganga. Leo wamenitumia ujumbe huu:
"Shemeji hii ndio namba ya yule mganga alienisaidia ana uwezo mkubwa sana wa kutoa mali bila kafara, kurudisha mke au mume PETE ya bahati na kutibu magonjwa yote. mpigie 0680261815"
Wewe mpigie tu, halafu unamuomba akukopeshe hela utamrudishia mwisho wa mwezi. Ila ujiandae kwa matusi.
 
Back
Top Bottom