Halotel mjitafakari mmebakia nyie

Halotel mjitafakari mmebakia nyie

Wahusika wa sms hizo ni wenyewe...sasa wataondoaje
 
Mkuu,

Unajuaje tatizo lipo Halotel?

Tanzania watu wanatoa namba sana, kila sehemu ukienda unaandika namba ya simu.

Vipi kama kuna watu wanazikusanya hizi namba na kuzitumia kwa mass marketing bila ya kupata namba kutoka Halotel?

Naelewa Halotel wanaweza kuweka anti spamming measures, lakini zaidi ya hapo kama watu wanatoa namba kirahisi yu, ukienda ofisi yoyote unawaachia namba yako, unajuaje kama hawauzi hizo namba?
Kweli sana sana halmashauri hizi huwa wanafanya huo mchezo sana
 
Yaani mimewaweka scam Hadi wale wanaotuma sms za kataa rushwa,

SIPENDI UPUUZI.
Wale wa kataa rushwa unawablock vp..
Aisee naumia ccm washenzi wanaonga watu alafu wanasema kataa rushwa
 
Habari ndugu wanajamvi.

nitoe pole pole za dhati kwa watanzania WOTE ,kutokana na msiba na janga La kuanguka kwa jengo La kariakoo.
Baada ya pole hiyo, nipende kutoa malalamiko YANGU kwenda kwa mtandao WA laini za simu, kampuni ya HALOTEL.

Kampuni hii imeshindwa kulinda wateja wake kwa kuruhusu ,watu tusio watambua kututumia meseji za UGANGA,KUJIUNGA FREEMASON,TUMA NAMBA HII,KUUNGANISHWA NA HUDUMA biła ridhaa yetu,mfano-HALOSOKA,na sms zingine zinazoendana na hizo.

Jambo hili La kupokea jumbe za namna hiyo kupitia laini ya halotel,limekuwa mara kwa mara likijitokeza na kuwa kero kwa baadhi yetu.

HII ni tofauti na mitandao mingine ambayo meseji za namna hiyo ni agharabu kuziona.

Natoa Lai kwa mtandao WA halotel ,kupambana kututatulia jambo Ili na kuzuia namba zetu kuweza kujulikana na watu hao wanaotutumia jumbe biła lidhaa yetu.

Asanteni
Sasa uwe na laini ya halotel na tigo kwenye simu moja hapo ndio utachoka zaidi. Unashangaa kwa siku unapata msg za hovyo zaidi ya 10. Vitangazo uchwara viko viiingi. Pumbafu kabisa.
 
Back
Top Bottom