dronedrake
JF-Expert Member
- Dec 25, 2013
- 23,901
- 58,103
sijui kwanini wanafanya ivyo, ila hakuna wizi wa MBsUshawah jiuliza kuna menu unaingia unakuta 1Gb kwa tsh 1000 na lain hio hio unaenda menu ingne unakuta 1Gb kwa buku jero π kwann? Huoni kuna moja imesetiwa haiesabu real 1GB
Mkuu nilidhani ni huku kijijini, majuzi nilitembelea rafiki yangu jijini Mwanza nimekuta napo hali ni vile vile; wamezima mtandao kabisa!Ttcl sijui inataka kujifia?
Maana kutopatikana kwa network Kwa masaa mengi limekuwa ni jambo la kawaida siku hizi [emoji848][emoji848]
Inauma sana.
Imagine mtu anataka huduma labda ya Bolt/Uber taxi aende hospitali lakini TTCL wamekata mtandao na hakuna mbadala wa usafiri mwingine si ni mtihani mkubwa huo?!
TTCL mnakwaza sana [emoji57][emoji57][emoji18]
Huwa unazima data unapokuwa hutumii internet au unajiachia tuu mkuu??Mimi nilijiunga kifurushi cha wiki kwenye kampuni fulani lakini ndani ya dakika moja nikaambiwa "kifurushi chako kimeisha" yaani within one hour toka ninunue kifurushi cha wiki.
Elfu 10 unapata GB ngapi kiongozi?Tumieni Zantel
Wanakata pesa??Niliachana nao baada ya kila nikiweka hela lazima wanakata salio langu bila hata sijatumia kwa namna yoyote
Funguka basi tujue huo wizi wao?Ficha upumbavu wako nimefanya kazi mtandao mmoja wa simu kitengo flani kwa mwaka mmoja najua wizi unaofanyika
Ushawah jiuliza kuna menu unaingia unakuta 1Gb kwa tsh 1000 na lain hio hio unaenda menu ingne unakuta 1Gb kwa buku jero [emoji16] kwann? Huoni kuna moja imesetiwa haiesabu real 1GB
Huna pa kukimbilia. Hao wote huwa wanakaa vikao ili wawanyonye kwa pamoja ili isije ikatokea mmoja wao akajifanya mwema sana akawaharibia wengine biashara.
Kila utakapokwenda wembe ni ule ule
KwMba technology kwenu ipo chini sana huwezi waza mtu ana set pale ikuoneshe 1Gb ila system imekupa labda mb 800?Funguka basi tujue huo wizi wao?
Hamieni airtel hamtojutia kwa kweliNilikuwa mtumiaji mzuri sana wa mtandao wa Vodacom. Baadae wakaja kupandisha bei za vifurushi vyao kwa kiwango kikubwa. Niliendelea kutumia Vodacom kwa matumizi yangu makubwa na kidogo laini ya Halotel. Baadae nikaja kushtuka Vodacom ukiwa mteja mzuri wanakupandishia bei, vifurushi vyako vinakuwa vya gharama zaidi kuliko wanaotumia kwa kusua sua. Nikaacha au kupunguza sana kuweka vocha na kununua bando kwenye Vodacom.
Nikahamia Halotel. Vifurushi vyao havikuwa na gharama sana kama Vodacom, ila speed yao ya intanet haikuwa na uwezo mkubwa kama Vodaocom lakini ilitosha. Karibuni hapa, nao wamepandisha bei za vifurushi nikaona wote ni wale wale. Kilichokuja kunishtua ni bando la halotel kuanza kuisha kwa haraka sana. Bando la wiki halimalizi siku moja. Gb 1 inaisha ndani ya muda mfupi mno kwa matumizi ya kawaida,nikaona kuna kitu hakipo sawa.
Nikasema ngoja nianze kutumia tena Vodacom, kuanzia juzi najiunga mabando ya Vodacom tu. Huwa nanunua vocha kutoka App ya NMB, bila intanet hununui vocha kwenye app. Kwa kuwa sasa nimeseti matumizi yangu yote kwenda laini ya vodacom, nikanunua vocha ya 1000 kwenye laini ya halotel ikae standby ili bando likikata kwenye voda nitumie hii buku kununulia vocha kwenye App ya NMB. Bila matumizi yeyote niliyofanya kwenye halotel asubuhi hii wamekata 200 kwenye ile buku niliyoweka standby, nakuta kuna Tsh 800 tu.