Nilikuwa mtumiaji mzuri sana wa mtandao wa Vodacom. Baadae wakaja kupandisha bei za vifurushi vyao kwa kiwango kikubwa. Niliendelea kutumia Vodacom kwa matumizi yangu makubwa na kidogo laini ya Halotel. Baadae nikaja kushtuka Vodacom ukiwa mteja mzuri wanakupandishia bei, vifurushi vyako vinakuwa vya gharama zaidi kuliko wanaotumia kwa kusua sua. Nikaacha au kupunguza sana kuweka vocha na kununua bando kwenye Vodacom.
Nikahamia Halotel. Vifurushi vyao havikuwa na gharama sana kama Vodacom, ila speed yao ya intanet haikuwa na uwezo mkubwa kama Vodaocom lakini ilitosha. Karibuni hapa, nao wamepandisha bei za vifurushi nikaona wote ni wale wale. Kilichokuja kunishtua ni bando la halotel kuanza kuisha kwa haraka sana. Bando la wiki halimalizi siku moja. Gb 1 inaisha ndani ya muda mfupi mno kwa matumizi ya kawaida,nikaona kuna kitu hakipo sawa.
Nikasema ngoja nianze kutumia tena Vodacom, kuanzia juzi najiunga mabando ya Vodacom tu. Huwa nanunua vocha kutoka App ya NMB, bila intanet hununui vocha kwenye app. Kwa kuwa sasa nimeseti matumizi yangu yote kwenda laini ya vodacom, nikanunua vocha ya 1000 kwenye laini ya halotel ikae standby ili bando likikata kwenye voda nitumie hii buku kununulia vocha kwenye App ya NMB. Bila matumizi yeyote niliyofanya kwenye halotel asubuhi hii wamekata 200 kwenye ile buku niliyoweka standby, nakuta kuna Tsh 800 tu.