Halotel ni wezi, wakimbieni!

Halotel ni wezi, wakimbieni!

clinician

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2014
Posts
2,098
Reaction score
4,926
Nilikuwa mtumiaji mzuri sana wa mtandao wa Vodacom. Baadae wakaja kupandisha bei za vifurushi vyao kwa kiwango kikubwa. Niliendelea kutumia Vodacom kwa matumizi yangu makubwa na kidogo laini ya Halotel. Baadae nikaja kushtuka Vodacom ukiwa mteja mzuri wanakupandishia bei, vifurushi vyako vinakuwa vya gharama zaidi kuliko wanaotumia kwa kusua sua. Nikaacha au kupunguza sana kuweka vocha na kununua bando kwenye Vodacom.

Nikahamia Halotel. Vifurushi vyao havikuwa na gharama sana kama Vodacom, ila speed yao ya intanet haikuwa na uwezo mkubwa kama Vodaocom lakini ilitosha. Karibuni hapa, nao wamepandisha bei za vifurushi nikaona wote ni wale wale. Kilichokuja kunishtua ni bando la halotel kuanza kuisha kwa haraka sana. Bando la wiki halimalizi siku moja. Gb 1 inaisha ndani ya muda mfupi mno kwa matumizi ya kawaida,nikaona kuna kitu hakipo sawa.

Nikasema ngoja nianze kutumia tena Vodacom, kuanzia juzi najiunga mabando ya Vodacom tu. Huwa nanunua vocha kutoka App ya NMB, bila intanet hununui vocha kwenye app. Kwa kuwa sasa nimeseti matumizi yangu yote kwenda laini ya vodacom, nikanunua vocha ya 1000 kwenye laini ya halotel ikae standby ili bando likikata kwenye voda nitumie hii buku kununulia vocha kwenye App ya NMB. Bila matumizi yeyote niliyofanya kwenye halotel asubuhi hii wamekata 200 kwenye ile buku niliyoweka standby, nakuta kuna Tsh 800 tu.​
 
TTCL sijui inataka kujifia?
Maana kutopatikana kwa network Kwa masaa mengi limekuwa ni jambo la kawaida siku hizi [emoji848][emoji848]

Inasikitisha sana.

Imagine mtu anataka huduma labda ya Bolt/Uber taxi aende hospitali lakini TTCL wamekata mtandao na hakuna mbadala wa usafiri mwingine si ni mtihani mkubwa huo?!

TTCL mnakwaza sana [emoji57][emoji57][emoji18]
 
Ttcl sijui inataka kujifia?
Maana kutopatikana kwa network Kwa masaa mengi limekuwa ni jambo la kawaida siku hizi [emoji848][emoji848]

Inauma sana.

Imagine mtu anataka huduma labda ya Bolt/Uber taxi aende hospitali lakini TTCL wamekata mtandao na hakuna mbadala wa usafiri mwingine si ni mtihani mkubwa huo?!

TTCL mnakwaza sana [emoji57][emoji57][emoji18]
Mitandao ya Tanzania uweledi ni sifuri
 
Niliachana nao baada ya kila nikiweka hela lazima wanakata salio langu bila hata sijatumia kwa namna yoyote
 
Back
Top Bottom