Kingine mtoa mada akae akijua unapokua na MB 100 afu uka download kitu cha MB 40 labda asitegemee zitatumika MB 40 zile zile ategemee MB 65 zitatumika, kuna sent & received data kutoka kwenye server na kukulink na kifaa chako hapo katikati kuna MB zinatumika.
Kuna Retry na Error Correction Kwenye mazingira dhaifu ya mtandao, kuna uwezekano wa kurudiwa upya (retries) na marekebisho ya makosa ya (error correction) ambayo yanaweza kuongeza matumizi ya data na wakati mwingine, faili huwa na compression dhaifu au zisizofanikiwa ku kucompressiwa vizuri na alie upload, hii inaweza kuongeza ukubwa wa data/MB zinayotumika uki download.
Tusipende kuwalaumu sana ISPs, kumbe kuna mambo ya kawaida kabisa ya kitech yanafanyika ili wewe ufurahie kuepo online [emoji28] kingine hata kama huoni kuna background tasks kwenye simu yako OS (hasa kama unatumia android) yenyewe tu inakula data ili ijiweke sawa kiutendaji.