Hama hama ya viongozi wa CHADEMA inarudisha nyuma hamasa ya vijana kuupambania upinzani

Wapinzani wanaweza kuuza mama zao kuingia madarakani.Walio madarakani wanaweza kuua ndugu zao ili wabaki madarakani.

This is the Scramble for and Partition of keki ya Taifa.

Raia shtuka,roho nzuri hailipi,wema haulipi, udini hailipi wala uadilifu haulipi.
Dunia hii inawazawadia wezi, waovu, waongo na wasaka tonge shibe na ukwasi for the rest of their natural lives.
Sankara yukwapi, Lumumba yukwapi??
 
Hao generation Z ndiyo chama chenyewe, maana wanaamini na kunia mamoja. Ni vile tu hawajasajiliwa na kuchagua viongozi wao.

Ideology ndiyo ndiyo huunda chama. Bila ideology hakuna chama
 
Lakini kwenye demokrasia haya mambo huwa yanatokea kwa maana kwamba kila mtu ana uhuru wa kuamua kufanya jambo ambalo linaleta amani na faraja katika maisha yake. Inabidi tu tuvumilie hali kama hii, lakini kwa upande mwingine tukiwa na upinzani tunapata balance: kuna mambo yatakayotoka upande huu na mengine upande ule, then ukiweka pamoja unapata kitu kamili. Hivyo, kuhama vyama ni jambo la kawaida kabisa.
 
Hapana mkuu. Siasa ni Imani. Mtu anapokuwa kigeugeu kwa kile anachoamini ujue kuna shida
Hata nawe kuna wakati unakuwa kigeugeu kwenye harakati zako maishani, hao wanasiasa ni wanadamu kama mimi nawe, msiwachukulie kama robots mnakosea, wanatimiza haki yao kisheria acheni kuwa madikteta kwa maamuzi binafsi ya wengine.
 
Mwalimu Nyerere aliliona hili jambo mapema sana na kulikemea akiwa bado CCM miaka ile ya 1990, angalieni ile clip yake ya “ malaya malaya” … labda mwenye kheri Nyerere huko alipo Anacheka tu na malaika zake…
 
Yaani huyu alikuwa anawatukana cc.m kila siku sasa huko ataenda kuongea nini jamani,alikuwa anawaita akili ndogo!
 
Kuna vitu vinasikitisha sana nchi hii.

Hakuna kitu kinakera kama ujinga huu wa kina Msigwa. Nimemdharau sana
Bora kuzaliwa paka ulaya utakuwa na akili kuliko wana siasa wa tz
 
Hivyo, kuhama vyama ni jambo la kawaida kabisa.
Kuhama chama kwa mtu ambaye ametangulizwa mbele kama kiongozi wa ideology (chama) inavunja maana na uwepo wa chama hicho.

Wahame wanachama wa kawaida hapo sawa.

Hebu angalia hii orodha ya waliohama:-Mashinji, Katambi, Dr. Slaa, na Msigwa. Mwanachama wa kawaida inakuwaje?
 
Ndiyo reality we have to cope with kwa sababu hatuwezi kuizuia. Si hata wengine huwa wanahama kutoka chama tawala? Kwa upande wangu, pamoja na kwamba natamani tuwe na strong opposition, lakini pia ndiyo aina ya watu wetu tulionao. So, we have to bear with them.
 
Uko sahihi. Hii hama hama inaonesha jinsi watanzania walivyo vigeugeu, hawasimamii kile wanachokiamini. Leo kasema hivi kesho anakikana. Wanaohama ni reflection ya tabia zetu watanzania.
 
Iko hivi, watu watapoteza hamasa kwa vyama vya siasa, lakini hakuna uwezekano wa kuondoa upinzani. Kwa hiki kinachoendelea kwa hizi hama hama kama za kina Msigwa, zinafanya watu wengi kupuuza siasa za vyama. Na kwa bahati mbaya sana hali hii haiwafaidishi hata ccm, bali kuzipuuza jumla siasa za vyama.
 
Uko sahihi. Hii hama hama inaonesha jinsi watanzania walivyo vigeugeu, hawasimamii kile wanachokiamini. Leo kasema hivi kesho anakikana. Wanaohama ni reflection ya tabia zetu watanzania.
Sure. Inabidi tujitafakari upya. Lakini recently nimejifunza to turn challenges into opportunities (not to allow negative things to hurt me). Au niseme to build on positive things I see in other people. Mara nyingi mambo ambayo ni hasi yanatawala nafsi zetu na yale positive yanakosa nafasi. Ni vigumu kuwa positive, lakini tukifaulu kufanya hivyo ni better kuliko kuwa negative au kuchukia.
 
Uko sahihi mkuu.
 
Uache kupambania maisha Yako uanze kupambania kina Mbowe na genge lake?
 
Anyway... huu sio wakati wa kukata tamaa tuendeleze Mapambano.✌️
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…