Hamad Masauni alifukuzwa UVCCM kwa kufoji Umri, Ni kejeli kwa Nchi kumteua kuwa Waziri

Hamad Masauni alifukuzwa UVCCM kwa kufoji Umri, Ni kejeli kwa Nchi kumteua kuwa Waziri

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Ili aendelee kuwa Mwenyekiti wa Uvccm hakutakiwa kuzidi umri wa Miaka 30 kwa utaratibu wa wakati ule (Niko tayari kusahihishwa), labda Wabadili kipindi hiki.

Baada ya kuona Umri unamtupa Mkono Bwana Masauni aliamua kufake umri kwa kuboresha taarifa za tarehe ya kuzaliwa kwake na kusogeza kutoka 1973 hadi 1979 (Hapa napo niko tayari kusahihishwa), Baada ya Mahasimu wake kujua hili wakamchoma, Akaondolewa kwenye kinyang'anyiro na kutimuliwa, Akaja kuokolewa na Kikwete kwa kuteuliwa Mbunge wa Viti maalum, Natumaini hakuna aliyesahau kashfa ile na Kama Masauni anabisha ajitokeze JF kubisha, Ushahidi kuhusu jambo hili umejaa hapa hapa JF.

Kwa kiongozi anayefoji mambo ili apewe kipaumbele hafai kuteuliwa popote, Na hasa kwenye Wizara nyeti kama ya Mambo ya Ndani, Hii yaweza kuwa sababu ya Hamad Masauni kushindwa Kuongoza wizara hii, Uwezo wake ni mdogo mno.

Soma Pia: Tafrani yazuka msibani Tanga: Waombolezaji wakataa dua ya Waziri Masauni wakimtaka ajiuzulu

Mwl Nyerere aliwahi kusema hivi, Nanukuu, "Kama unampenda mtu kwa sababu ya sura yake basi nenda kanywe naye Chai, Mwisho wa kunukuu.
 
Nawasogezea uzi 😏

Again CDM you're not fighting people. you're fighting a system. tuna uhakika hata akija waziri mwingine, haya mambo yataendelea kama kawaida. Muda umetufundisha hili.
 
Again CDM you're not fighting people. you're fighting a system. tuna uhakika hata akija waziri mwingine, haya mambo yataendelea kama kawaida. Muda umetufundisha hili.
Mfumo unaongozwa na watu, huwezi kuangusha mti mkubwa bila kupruni matawi kwanza
 
Mfumo unaongozwa na watu, huwezi kuangusha mti mkubwa bila kupruni matawi kwanza
Kwani nyie si mlipiga majungu sana Simon Sirro kwamba ndiye tatizo?..je baada ya kuondolewa kwake mwenendo wa jeshi la polisi una nafuu yoyote?.....ukweli ni kwamba nyinyi mnaojiita WAPINZANI ni WAPUMBAVU msio na chembe ya AKILI ndio maana CCM wanawatendea vyovyote vile watakavyo
 
Hoja yako ni ya kijinga
 
..unadhani walipaswa kumlaumu nani?
 
Masauni ajiuzulu ndio kama waziri mwenye dhamana lakini tatizo la haya yote wala sio masauni.
Kuna asilimia nyingi masauni akawa hajui chochote au anajua lakini ni suala ambalo lipo nje ya uwezo wake.

IGP na DGIS hawa ndio wakuchukua lawama na wanatakiwa wawe walengwa wakuu kwa kutueleza kila kilichotokea, hawa ndio walengwa wakuu kuliko hata masauni huyo.

Tukio limetokea kweupe tena kwenye gari liliobeba abiria na si gari la mtu binafsi ni public transport kwahiyo hili sio tukio la ujambazi , taarifa za awali zinaeleza waliomchukua walijatumbulisha kama ni polisi na uzuri tunaambiwa kulikua na askari ndani ya gari hii yote inaonyesha tukio halijafanywa na random people bali ni mamlaka husika.

Majibu yanapatikana sehemu mbili tu hapa na ndipo tunapotakiwa tutafute majibu yetu kwa jeshi la polisi likiongozwa na IGP pia kwa usalama wa taifa likiongozwa na DGIS, kwa njia yoyote ile hizi sehemu mbili ndizo zenye majibu .
Inawezakana polisi wanajua ila kutokana na kuzidiwa nguvu na( wenzao) wakaona hili suala lipo nje ya uwezo wao au wakawa hawajui kabisa kutokana na (wenzao) waliamua kuliratibu wao kama wao .

Tunahangaika na masauni bure tu japo kujiuzulu kwake hakuepukiki lakini masauni sio mwenye majibu na hili suala .
Majibu yapo kwa TISS na PT hawa ndo wakuwajibika zaidi iwe IGP au DGIS .
 
..unadhani walipaswa kumlaumu nani?
Kabla sijakujibu,pitia tena kuna sehemu nimeuliza hapo..... baada ya Sirro kuondolewa je kuna mabadiliko yoyote chanya kwenye mwenendo wa polisi ?....jibu lake litakusaidia walau
pa kuanzia...

na vile vile KULAUMU inasaidia nini? Kwani mmeshalaumu wangapi na Mara ngapi?

Nikisema wapinzanI wenye nafasi za juu kwenye nchi hii ni sehemu ya TATIZO sitokuwa SAHIHI?
 
Back
Top Bottom