Hamad Rashid Mohammed naye kuondoka CUF!

Zitto nimependa sana flexibility uliioonyesha hapo mwisho, "only fools never change their minds.." huu ni wakati ambao watawala wameonekana wameshindwa nchi na kila mtu ameona, kuna kipindi jana kilirushwa ITV kuhusu wananchi waliobomolewa nyumba zao Dodoma...wanvyoongea unapata hisia kama watu wameamka...wanaona udhalimu, ufisadi, uonevu, kiburi na jeuri ya walioko madarakani...uongozi mbadala ni muhimu sana...na chadem imekuwa katika nafasi nzuri..let us use it...nimeshaihakikishia chadema jimbo moja 2005...kwahiyo mchango wako kwa wakati kama huu ni muhimu sana..kama uliamua kuitumikia nchi yako, wananchi wamekupokea kwa mikono 2...kuondoka ni sawa na kuwacheza shere....i will suport u if you change your mind and everyone else will do....
 
Nimefurahi sana maelezo ya Mh Zitto..
Sasa Hamad Rashid anaenda chadema? kule pemba utamweleza nini mtu kuhusu Cuf? Tambwe sasa anasema uongo mtupu,kule Bukoba tumeskia Lwakatare naye tayari anazungumza uongo mtupu,sasa na Hamad Rashid ataweza kuongea uongo? ninavofahamu mimi kwa historia iliyopo ukitoka Cuf kama umejilani mwenyewe,tumeona Mapalala,nyaruba,ramadhan mzee,salum msabah,tambwe wako wapi hivi sasa,unajua ukiwa mkweli utang'aa na ukiwa mnafiki ipo siku utakwisha tu.. kama mimi siamini kama anaweza kutoka Cuf,na si yeye pekee,kwa upande wa znz wananchi kule wana uhakika na baadhi ya watu wao ktk Cuf kwa upande wa znz,kwa mfano Hamad rashid,Maalim seif,nasor khamis,abubakar khamis,Machano,juma duni na wengine wametangulia mbele ya hakki,hawa watu wameapishana kuwa watakuwa wapo pamoja ktk kuitetea znz mpaka mauti yao yawafike.. SASA HII HABARI SIJUI MAANA HUMU NDANI TUMEINGILIWA HIVI SASA,INAWEZEKANA LABDA,ACHA TUONE..
 
Calipso Mapalala walimchukua kiadvantage akina seif Mapalala aliwaamini akijua kuwa watamuenzi wakamgeuka bwana ,Mapalala alikuwa mwana mageuzi kweli
 
Froida..
Fatilia uzuri historia ndugu yangu usiongee kwa mawazo yako,unajua kilichomuondosha mapalala.. labda ujaribu kuwauliza wenye kujua then utapata jawabu zuri,kwa ufupi alianzisha upinzani ndani ya chama baada ya kutumiliwa na watu.. na hapo ndio akaja Mzee musobi mageni kama unamjua,mzee wa heshima zote.
 


Mimi siamini kama hii habari ya kuhama ni kweli, lakini pia sikubaliani iwapo Hamad Rashid ata-make a good leader in CUF. Alinichomoka pale alipomuuliza Pinda Bungeni kuhusu suala la Mengi kuwataja mafisadi papa -- yaani serikali ichukue hatua gani dhidi ya Mengi -- yaani yale yale ya Profesa yaliyompotezesha hadhi alipojitokeza hadharani kuwatetea "mapapa" wa ufisadi na kumponda Mengi..

Nadhani jibu la Pinda -- kwamba "mapapa" wale wana uhuru kwenda mahakamani wakipenda -- bila shaka lilimkata Hamad Rashid maini, na kuonekana a little bit silly.
 
Chadema imeshakuwa CCMB, dalili ndiyo hiyo badala ya recruite wanachama wapya na kuwapandisha wanachama wako vyeo, wanabaki kuchukua wananchama wanaohama...hii dalili ya kuanza kufilisika
a)Hivi chadema haina mwanachama anafaa urais mpaka atokee CUF au CCM??
b) Chadema imekuwa inatega watu waondoke toka vyama vingine tangu zamani unakumbuka waliacha kumweka mgombea urais kwa muda 2000 wakitega kina Kikwete wakitupwa wajiunge?
c) Bado sana CCMB, wenye akili tunaona ujinga wao!, sasa wanamsubiri hamad aje aongoze ama kweli mmeishiwa kwelikweli, hakuna system ya kupata viongozi mpaka aje kutoka nje?
 
Watoke wote basi ikibakia bendera tu bado CCM watakuwa hawako salama huko Nchini Pemba ,maana tatizo la huko sio nani yupo na hayupo CUF bali tatizo sugu la huko ni kuwa CCM haifai tena kuwepo madarakani,muhula wa kuongozwa na viranja na mafisadi wa CCM umefikia tamati,hawana tena nafasi katika mioyo ya WaPemba walio wengi sana ,hivyo atoke Lipumba ,aondoke Seif na mwengine yeyote yule basi bado CCM itakuwa na wakati mgumu zaidi kuzidi huu walio nao,yaani hata CUF ikisambaratika na kubaki bendera ,hilo halitowageuza wananchi kuichagua CCM ,haja ya wananchi ni kuona CCM inaondolewa madarakani na huo ndio msingi wa demokrasia wananchi kuwa na chaguo lao msimamo ambao umetoa chaguo la WaPemba kuwa na nchi yao ,sasa isije kuwa kujiengua huko ni kuanza safari Rasmi ya kuipigania Pemba kikamilifu ,huwezi kujua.
 

chadema kina fanya vizuri kwa hiyo kila mtu anataka ku join bandwagon
 

Mheshimiwa Shukrani kwa majibu yako mazuri,na ufafanuzi wa dhati kuhusu imani yako kwa Chadema,Lakini pia kuwa makini katika kujibu Mabandiko yanayokuhusu,na kumbuka kwamba si kila Bandiko linahitaji majibu yako,hata kama linakuhusu wewe binafsi.

Kuna mabandiko yanawekwa kwa nia nzuri na mengine yapo kwa nia ya kukejeli.....Hakuna mtu atakayekupangia unapaswa kufanya nini katika maisha yako ya siasa...Lakini kumbuka kuwa "Watanzania wengi bila kujali Itikadi za Vyama wana Imani na wewe".Katika muda wote uliokaa Bungeni umekuwa Mtetezi mkubwa wa Watanzania kwa maana hiyo maamuzi yako yafanye kwa kujali maslahi ya walio wengi.

Wengi humu tunakuchukulia Zitto kama kiongozi wa Watanzania na hatukuoni Zitto kwa kofia yako ya Uchadema......Kumbuka maneno yako Mheshimiwa "Utaifa kwanza"
 
Sasa na wewe unataka waende wapi watu hawa??
 
habari hii haina ukweli,na PRACTICALLY HAIWEZEKANI

kuhusu ZITTO!well,mimi namshauri aachane na siasa.he has proved himself 'SELFISH and UNSTABLE' kwenye sakata la dowans!

GO AWAY ZITTO!someone else will take the lead!YOU ARE TASTELESS NOW
 
habari hii haina ukweli,na PRACTICALLY HAIWEZEKANI

kuhusu ZITTO!well,mimi namshauri aachane na siasa.he has proved himself 'SELFISH and UNSTABLE' kwenye sakata la dowans!

GO AWAY ZITTO!someone else will take the lead!YOU ARE TASTELESS NOW
We itakuwa CCM.
 

Nimefurahi kusikia kuwa CUF imekimbiwa na viongozi wengi kiasi hicho! Na bila shaka na malaki ya wanachama pia na ni sababu tosha ya chama kupoteza umaarufu wake hasa kwa Chadema.

Nyie katika CUF msianze kutafuta visingizio – eti CCm inashirikiana na Chadema kukikandamiza kwa sababu ni tishio na hivyo Chadema inakwezwa ili iwe No 2 kutoka CCM.

Tishio? Labda Visiwani tu, na kama huku Bara, basi tishio hilo angalau lilikuwa kweli mwaka 2000 ikilipofanikiwa kuipiku NCCR katika nafasi ya pili kwa kura.

Lakini sasa hivi kinaporomoka kwa kasi – wazungu wanasema “free-fall” na tutegemee wengi kukihama chama hicho – ingawa siamini iwapo hamad Rashid ni mmoja wao. Ushahidi wa kuporomoka ni Busanda – CUF iliambulia kura 900 tu ni karibu asilimia 5 ya kura walizopata Chadema!

Acheni kuilaumu Chadema kwa hilo, kila chama kiweke mbinu zake za kushinda uchaguzi na kama mbinu hizo ni kinyume cha sheria basi vyenyewe vyama vitajiju. Kama huwezi kuweka helikopta – hakuna haja ya kukiponda chama chenye kuweka helikopta. Kuna baadhi ya wanaCUF wanasema eti hiyo helikpta ya Chadema ni mchango wa CCM. Kwa nini wenyewe CCm wanapata kiwewe cha helikopta iwapo ndiyo wao waliwapa?

CUf wanashindwa kujibu tuhuma kama ilivyoripotiwa kwamba kuna kigogo kimoja cha CCM kinaifadhili CUF – na inasemekana kigogo huyo ni RA Fisadi na 1. Kwa hali hii – kwanini msikimbiwe?

Ingawa hakuna ushahidi mzito kuhusu ufadhili huu, lakini upo wa kimazingira ambao una nguvu kidogo – Profesa alipojitosa kwa nguvu kuwatetea ”mapapa” waliotajwa na Mengi.

Jee aliagizwa kufanya hivyo – kwa kulipa fadhila za ufadhili? Pia kuna uhusianio wa karibu sana baina ya RA na Jussa – jee huu umeelezwa sasawa? WanaCUF wanapohoji haya wanaengulwa!

Lwakatare bila shaka ni mmoja wao na kama unavyosema kaanza kusema uongo – basi uongo huo umesadia kukomba maelfu ya WanaCUF huko Bukoba waliojiunga na Chadema.


 
Hatuna haja ya kubishana sana kwani sote tunaweza kuwa hatujui kinachoendelea katika mawazo, akili na nafsi yake. ila nachoweza kusema ni kuwa SIKU IKIFIKA yote yatakuwa wazi na itakuwa ni mwisho wa tetesi na kujenga hoja ambazo sisi sio waamuzi wake, ya Lwakatare wengine hawakuamini lakini ikawa kama ilivyotabiriwa so we better have some little uvumulivu n wait.
the resource time will prove it wrong or sawa.
 

Conservative wa nini??
Amini nakuambia hakuna mwanasiasa yeyote Tz ambaye ni ni Conservative wote wapo kwa malengo yaleyale ,nia ile ile ,sababu zilezile ,ufahamu uleule,mwongozo uleule ,utashi ule ule na miujiza zile zile.
 

Halafu unajiita mwana mageuzi
 
Conservative wa nini??
Amini nakuambia hakuna mwanasiasa yeyote Tz ambaye ni ni Conservative wote wapo kwa malengo yaleyale ,nia ile ile ,sababu zilezile ,ufahamu uleule,mwongozo uleule ,utashi ule ule na miujiza zile zile.
Duh! mkuu hii nzito kichizi inabidi nichukue muda kuitafakari kabla sijameza!..
 

Nani mwenye hati miliki ya wanachama?
 

Tunakujua wewe ni sisi Maf............. wewe ndiye nenda huko utachie Zito wetu. He is a hero
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…