Hamas inashauriana na vikundi vingine vya Palestina juu ya mpango wa kusitisha mapigano

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Hamas inasema inashauriana na makundi mengine ya Wapalestina kabla ya kutoa jibu rasmi kwa pendekezo la hivi punde la usitishaji vita upya huko Gaza na kuachiliwa kwa mateka lililotolewa na Marekani.

Rais Donald Trump alisema Ijumaa asubuhi kwamba alitarajia kujua ndani ya saa 24 ikiwa Hamas imekubali mpango huo.

Siku ya Jumanne, Trump alisema Israel imekubali masharti ya msingi ya kusitisha mapigano kwa siku 60, ambapo pande husika zitashiriki katika kumaliza vita vya miezi 20.

Wakati huo huo, jeshi la Israel linaendelea kushambulia kwa mabomu maeneo yote ya Ukanda wa Gaza.

Waandishi wa habari wa eneo hilo waliripoti kusikia milipuko na milio ya risasi huku helikopta za Israel zikishambulia eneo la kusini la Khan Younis siku ya Ijumaa asubuhi.

Usiku kucha, takriban Wapalestina 15 waliuawa katika mashambulizi kwenye mahema mawili ya watu waliokimbia makazi yao huko Khan Younis, hospitali ya eneo la Nasser ilisema.

Jeshi la Israel bado halijatoa tamko lolote kuhusu mashambulizi hayo, lakini limesema vikosi vyake "vinafanya kazi ya kumaliza uwezo wa kijeshi wa Hamas".
 
hivi kobazi si mlisema Hamas wameshinda vita sasa vilio vya nini kwa mmyahudi aliyeshindwa vita
 
Back
Top Bottom