Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Yule msemaji asiyechoka wa Hamas aitwaye Abu Ubeida amesema tangu mwezi Juni mwaka huu wamebadili mfumo wa kuwalinda mateka na kutoa maagizo hayo kwa wanaowalinda pindi askari wa Israel wanapokaribia kuwafikia.Hata hivyo hakutoa ufafanuzi wa mfumo huo.
Inakumbukwa mnamo mwezi Juni jeshi la Israel lilifanikiwa kuwaokoa mateka 4 katika moja ya tukio la kikatili la uokoaji ambapo raia zaidi ya 100 wa Palestina waliuliwa.
Hapo juzi jumla ya mateka 6 miongoni mwa mateka waliobaki Gaza walikutwa wakiwa wamekufa katika hali iliyoonesha kupigwa risasi.Baada ya jeshi la Israel kutoa tangazo hilo kumetokea maaandamano makubwa zaidi yakimtaka waziri mkuu wa nchi hiyo kufikia makubaliano na Hamas ili kusitisha vita.
Akizungumza kupitia televisheni baada ya maandamano kuwa makubwa na kutishia kuiathiri nchi zaidi kiuchumi kutokana na vyama vya wafanyakazi kutishia kufanya migomo, Netanyahu ameomba radhi kwa tukio hilo la kuuliwa kwa mateka hao,hata hivyo amerusha lawama kwa Hamas jambo ambalo waandamanaji wanapingana naye.
Kwa upande mwengine wachambuzi wa mwenendo wa vita vya Gaza wameweka wazi kuwa maelezo yanayotolewa na Marekani na lawama kwa Netanyahu hayaendani sawa na uzito wa hali ya vita na wala hakuna dalili ya kusaidia kumaliza vita hivyo kwa njia ya majadiliano ambayo mara kadhaa yamekuwa yakionekana kufikia mwisho huku Netanyahu akibadili hadidu rejea za makubaliano yaliyofikiwa inapokuja muda wa kutiliana saini.
Hivi karibuni kwa upande wao Hamas wamesema hawana haja tena na mazungumzo mapya ya kusitisha vita bila kutekelezwa yaliyoafikiwa kabla