Hamis Mgeja adai kuna waliopandishwa vyeo kwa sababu ya ‘kumtukana Lowassa’

Mgeja hakuwahi kumsaliti Edo. Kila alipokuwepo, naye alikuwepo!
Tofauti na "MSALITI" King Msukuma!
Msukuma ni mzee wa FURSA + WIZI..alisema mwenyewe akiwa Star tv,kwamba alikuwa akibebeshwa dhahabu mwilini,na kuvusha kwenda Kenya,..kwa kuwa alikuwa na kamwili kadogo,Askari hawakumuhisi kama ana mzigo,..HAFAI
 
Mgeja anaamini hao vijana (BAVICHA) wangeruhusiwa kweli hiyo 2015, wangeingia barabarani?😁.

2020 walihamasishwa kabisa kuingia road na yule jamaa ila wakayeyuka!

Lowassa hakuwa na mihemko, alikuwa na picha halisi ya waomba ruhusa hivyo akajua ni ndezi tu wanaomchora.
 
Ameyasema hayo alipozungumza na gazeti la Mwananchi kufuatia Msiba wa Rafiki yake Lowassa

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Sinyanga na rafiki wa karibu wa Hayati Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, Hamisi Mgeja amesema kiongozi huyo alikuwa na uvumilivu wa hali ya juu kiasi cha kuwasamehe waliomtukana.

Akizungumza kwa simu na Mwananchi leo Februari 10, 2024, Mgeja amesema, “Lowassa alikuwa mvumilivu sana, alitukanwa na alibezwa na kuna watu walipandishwa vyeo kwa sababu ya kumtukana, lakini hakuwajibu, bali alisema wasameheni kwa kuwa hawajui watendalo."

Akifafanua kuhusu uvumilivu huo, Mgeja amekumbuka uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ambao Hayati Hohn Magufuli wa CCM alitangazwa mshindi kwa kupata zaidi ya asilimia 58 ya kura, Lowassa aliyepata zaidi ya asilimia 39 aliwazuia vijana waliopinga matokeo hayo.

“Baadhi ya vijana ambao hawakuridhishwa na matokeo yale, walikusanyika wakamwambia tunasubiri ruhusa yako tuingie barabarani.

“Lakini yeye kwa busara zake akawaambia wavumilie kwa matokeo yale na kwamba hayuko tayari kuingia Ikulu mikono ikiwa imejaa damu,” amesema Mgeja.
Haya mambo ya eti vijana walitaka kuingia mtaani wakaambiwa watulie huwa inanikera kweli. Muwe mnaambizana uchochoroni!
 
Ameyasema hayo alipozungumza na gazeti la Mwananchi kufuatia Msiba wa Rafiki yake Lowassa

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Sinyanga na rafiki wa karibu wa Hayati Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, Hamisi Mgeja amesema kiongozi huyo alikuwa na uvumilivu wa hali ya juu kiasi cha kuwasamehe waliomtukana.

Akizungumza kwa simu na Mwananchi leo Februari 10, 2024, Mgeja amesema, “Lowassa alikuwa mvumilivu sana, alitukanwa na alibezwa na kuna watu walipandishwa vyeo kwa sababu ya kumtukana, lakini hakuwajibu, bali alisema wasameheni kwa kuwa hawajui watendalo."

Akifafanua kuhusu uvumilivu huo, Mgeja amekumbuka uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ambao Hayati Hohn Magufuli wa CCM alitangazwa mshindi kwa kupata zaidi ya asilimia 58 ya kura, Lowassa aliyepata zaidi ya asilimia 39 aliwazuia vijana waliopinga matokeo hayo.

“Baadhi ya vijana ambao hawakuridhishwa na matokeo yale, walikusanyika wakamwambia tunasubiri ruhusa yako tuingie barabarani.

“Lakini yeye kwa busara zake akawaambia wavumilie kwa matokeo yale na kwamba hayuko tayari kuingia Ikulu mikono ikiwa imejaa damu,” amesema Mgeja.
WENGI SANA HATA MAJINA YA VYEO WALIVYOPANDISHWA VINAJULIKANA
R.I.P LOWASSA wewe ni RAIS wa Mioyo ya Watanzania MUNGU akupe Pumziko Stahiki
 
Back
Top Bottom