Hamis Mwinjuma(Mwana FA) akutana na Wakuu wa Idara Muheza

Hamis Mwinjuma(Mwana FA) akutana na Wakuu wa Idara Muheza

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Mbunge wa Muheza, Hamis Mwinjuma (MwanaFA) amekutana na Wakuu wote wa Idara na vitengo ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Muheza katika kikao alichokiitisha kwa wilayani humo.

Lengo kuu la kikao ilikua ni pamoja na kuweka mikakati ya pamoja na kujadili changamoto zinazojitokeza kwenye Majukumu ya kila siku ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Muheza.

Katikati ya Kikao hicho cha Mwana FA na watendaji wenzake walipata ugeni wa ghafla wa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Bw Rajab Abdulrahman ambapo aliwasalimia na kuacha nasaha zake ikiwa ni katika kuhakikisha ilani ya Chama cha Mapinduzi, Chama chenye dhamana ya kuwatumikia wananchi kwa sasa, inatekelezwa kwa ufanisi.

Wengine ni waliohudhuria Kikao hiki ni pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri na Sektetarieti ya CCM ya Wilaya ikiongozwa na Katibu wa CCM wilaya Ndugu Simon Leng’ese.

IMG-20230110-WA0204.jpg
IMG-20230110-WA0207.jpg
IMG-20230110-WA0211.jpg
IMG-20230110-WA0204.jpg
IMG-20230110-WA0206.jpg
IMG-20230110-WA0195.jpg
IMG-20230110-WA0207.jpg
IMG-20230110-WA0201.jpg
IMG-20230110-WA0210.jpg
IMG-20230110-WA0193.jpg
IMG-20230110-WA0211.jpg
 
Kama kina posho sawa kama hakuna posho ni kuchoshana tu, wakuu wa idara wako chini ya mkurugenzi na wanawajibika kwa mkirugenzi, yeye kiherehere tu cha kutafuta cheap populality.
 
Kama kina posho sawa kama hakuna posho ni kuchoshana tu, wakuu wa idara wako chini ya mkurugenzi na wanawajibika kwa mkirugenzi, yeye kiherehere tu cha kutafuta cheap populality.
Umenena vema, mie ningekuwa mkuu wa idara sihudhurii huo upuuzi wa mbunge.
 
Wabunge feki wa mwendazake !! dunia hii aisee
 
Ni wakati muafaka kwa CCM chini ya mama Samia kuinua vijana wenye akili na uzalendo wa kweli kukijenga chama upya. Hawa wa sambuli hii ni kuwatokomeza kama mbung'o.
 
Haya yalitakiwa yafanyakie katika vikao vya baraza la madiwani la Halmashauri.
 
Back
Top Bottom